Tangazo

August 10, 2012

Airtel yafuturisha Wafanyakazi wake wa Kitengo Huduma kwa Wateja

Pichani ni Bi. Anethy Muga na Bw. Godfrey Kavishe, wote ni viongozi wa kitengo cha huduma kwa wateja katika Kampuni ya simu za mikononi Tanzania, Airtel, wakijumuika pamoja na wafanyakazi wa Kampuni hiyo katika futari iliyoandaliwa na kitengo hicho katika ukumbi uliopo ndani ya makao makuu ya Kampuni hiyo yaliyopo jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa Kampuni ya simu za mkononi Tanzania, Airtel, wakiwa wamejipanga kupata futari iliyoandaliwa na kitengo cha huduma kwa wateja cha Kampuni hiyo katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani. Hafla hiyo ilifanyika katikati ya wiki hii katika ukumbi uliopo ndani ya makao makuu ya Kampuni hiyo jijini Dar es Salaam.


Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya simu za mkononi Tanzania, Airtel, kwa pamoja wakila na kufurahia futari iliyoandaliwa na kitengo cha huduma kwa wateja cha Kampuni hiyo katikati ya wiki hii katika ukumbi uliopo ndani ya makao makuu ya Kampuni hiyo yaliyopo jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya simu za mkononi Tanzania, Airtel, Bw. Sam Elangaloor akila na kufurahi pamoja na wafanyakazi wa Kampuni hiyo katika futari iliyoandaliwa na kitengo cha huduma kwa wateja cha Kampuni hiyo katika ukumbi uliopo ndani ya makao makuu ya Kampuni hiyo jijini Dar es Salaam katikati ya wiki hii.

Wa tatu kutoka kushoto ni Bi. Adriana Lyamba Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja wa Airtel, akiwa na mameneja wengine katika picha ya pamoja baada ya futari iliyoandaliwa na kitengo cha huduma kwa wateja cha Kampuni hiyo kwa wafanyakazi wake. Hafla hiyo ilifanyika katikati ya wiki hii katika ukumbi uliopo ndani ya makao makuu ya Kampuni hiyo yaliyopo jijini Dar es Salaam.Pia Kampuni ya Airtel Tanzania leo imeendaa hafla fupi ya futari kwa wateja wake itakayofanyika ndani ya ukumbi wa Serena jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuwatakia Ramadhani Kareem wateja wake wote waliopo ndani ya mfungo huu mtukufu wa mwezi wa Ramadhani.
Wiki iliyopita Airtel ilifuturisha wateja wake waliopo jijini Arusha.

No comments: