Tangazo

August 27, 2012

Mkutano wa Kimataifa wa Mabadiliko ya Tabia Nchi waanza mjini Bangkok Thailand

Mwanasheria kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi Magreth Meela (kulia) na Bi Fauzia  Mwita Mkurugenzi wa Idara ya Sera, Mipango na Utafiti,ambae pia ni mwenyekiti wa kamati ya wataalam ya mabadiliko ya tabia nchi kutoka Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais - Zanzibar wakiwa katika Mkutano wa Mabadiliko ya Tabia Nchi Mjini Bangkok. (Picha na Evelyn Mkokoi) 
*******************
NA EVELYN MKOKOI
AFISA HABARI -OMR

Mkutano wa Kimataifa  wa mabadiliko ya Tabia nchi umeanza Nchini Thailand mjini Bangkok kama mkutano wa maandalizi ambapo, kundi la nchi za Africa zimekutana na kujadili mambo mbali mbali ikiwa ni pamoja na namna ya kukabiliana na kuhimili  mabadiliko ya tabia nchi.

Kundi hilo la nchi za Afrika, Likiongonzwa na uwenyikiti toka nchini Swazland, pia unategemeea kupata taarifa ya mikutano mbalimbali iliyofanyika baada ya ule uliofanyika mjini Bonn mwezi May 2012.

Suala la kuhimili mabadiliko ya tabianchi bado limejitokeza kuwa ni kipaumbele kwa nchi hizo za afrika. 

Tanzania ambayo ni waratibu wa masuala ya hasara na madhara yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi kwa niaba ya Afrika, iliwasilisha ripoti ya mkutano wa wataalam uliofanyika Nchini Ethopia mwezi Agosti 2012 uliohusu hatua zinazofaa kumudu hasara na madhara yatokanayo na mabadiliko ya tabi nchi, ambapo Sudan imegusia suala la muendelezo wa washiriki katika mikutano hii ili kuweza kupata michango mizuri ya mawazo  na kitaaluma wakati wa majadiliano katika mkutano huo kutokana na yaliyojitokeza Ethipia ambapo wataalam wengi hawakushiriki.

Mkutano wa mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika mjini Durban mwaka 2011 ulikubaliana kuanzishwa kwa chombo cha (ADP) ambacho, kitakachosimamia majadiliano ili kupata mkataba mpya utakaohusisha nchi zote katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia  nchi.

Mkutano huu wa Bangkok ndiyo mwanzo wa mchakato wa utekelezaji wa (ADP) ambapo unatakiwa ukamilike kabla ya mwaka 2015, Mkutano huu, unategemea kusikia na kujua, chombo hicho  kitafanya nini katika malengo yake ya kuhimili na kukabilianana mabadiliko ya tabia nchi, kupunguza gesi joto, kujenga uwezo katika eneo hilo pamoja na masuala ya sayansi na teknolojia na masuala ya fedha kugharamia masuala ya mabadiliko ya tabia nchi.

Wakati huohuo, Kundi la nchi za Afrika pia limegusia kuhusu, mkutano mkubwa wa masuala ya mazingira utakaohusisha mawaziri wa mazingira kutoka nchi za Afrika utakaofanyika mjini Arusha mwezi Septemba, ambapo wataalam watapata nafasi ya kujadili nafasi ya Afrika katika suala zima la mazingira ikiwa ni pamoja na  kipengele cha mabadiliko ya tabia nchi kuelekea mkutano wa dunia wa mabadiliko ya tabia nchi utakaofanyika mjini Dhoha mwezi disemba mwaka huu.

No comments: