Tangazo

August 13, 2012

UTOROSHWAJI WA WANYAMAPORI KIA: MAOFISA WATATU WA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII WATIMULIWA KAZI


Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu uamuzi wa Serikali wa kuwafukuza  kazi  watumishi watatu wa wizara hiyo kutoka na ukiukaji wa sheria na utekelezaji wa majukumu yao ya kazi kufuatia sakata la usafirishaji wa wanyama pori  kupitia Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro kwenda Quatar.Picha na Anna Nkinda wa MAELEZO
Wizara ya Maliasili na Utalii imechukua hatua za kinidhamu kwa watumishi wake tisa (9) kufuatia kadhia ya utoroshaji wa Wanyamapori Hai katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) na masuala mengine yanayohusu Wanyamapori. Watumishi hao wamechukuliwa hatua husika kufuatia kukamilika kwa uchunguzi wa tuhuma zilizokuwa zikiwakabili.

(1) Waliofukuzwa kazi kutokana na ukiukaji wa sheria katika utekelezaji wa majukumu yao ni:

    - Bw. Obeid F. Mbangwa         -    Mkurugenzi wa Wanyamapori. Wakati wa kadhia hiyo alikuwa             Mkurugenzi Msaidizi Matumizi ya Wanyamapori,

     - Bw. Simon Charles Gwera – Ofisi ya Uwindaji wa Kitalii – CITES na Utalii wa Picha Arusha,

     - Bw Frank Mremi - Ofisi ya Uwindaji wa Kitalii – CITES na Utalii wa Picha Arusha.

(2) Aliyeondolewa Cheo cha Madaraka kutokana na kutochukua hatua kamilifu za ulinzi ambazo zingeweza kuzuia kutokea kwa tukio la utoroshwaji wa wanyama ni:

    - Bw. Bonaventura M.C. Midala – Mkurugenzi Msaidizi, Undelezaji Wanyamapori. Wakati wa tukio alikuwa Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Kuzuia Ujangili.

(3) Wafuatao ni Maafisa Wanyamapori Daraja la II waliotekeleza maelekezo ya Wakuu wao wa kazi yaliyo kinyume cha Sheria ambao wamepewa Onyo Kali la Maandishi:

  - Bibi Martha P. Msemo       -        Afisa Leseni, Ofisi ya Uwindaji wa Kitalii, CITES na Utalii wa Picha Arusha.

    - Bibi Anthonia Anthony – Afisa Leseni, Ofisi ya Uwindaji wa Kitalii, CITES na Utalii wa Picha Dar es Salaam.

(4) Bw. Silvanus Atete Okudo ni Mkuu wa Kituo cha Uwindaji wa Kitalii, CITES na Utalii wa Picha Arusha aliyeshindwa kufuatilia kupata maelekezo ya Mkurungezi wa Wanyamapori kuhusu mtumishi wake aliyekiuka Sheria katika utoaji wa vibali. Aidha, alishindwa kupeleka kwa Katibu Mkuu taarifa kuhusu mtumishi huyo ili achukuliwe hatua za nidhamu.

    - Silvanus Atete Okudo – amepewa Onyo Kali la Maandishi.

(5) Wafuatao ni Maafisa ambao uchunguzi dhidi yao unaendelea:

    - Bw. Mohamed Madehele – Ofisi ya Matumizi Endelevu ya Wanyamapori

    - Bibi Mariam Nyallu – Kituo cha Uwindaji wa Kitalii, CITES na Utalii wa Picha – Arusha.

Wahusika wengine katika kadhia hiyo wasiokuwa waajiriwa wa Wizara ya Maliasili na Utalii watachukiliwa hatua na mamlaka nyingine husika.

[MWISHO]

Mhe. Khamis Suedi Kagasheki

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII

13 Agosti 2012



(Imetolewa kwenye Press Conference iliyofanyika Katika Viwanja vya Bunge Dodoma tarehe 13 Agosti 2012)

No comments: