Tangazo

September 14, 2012

AIRTEL TANZANIA NA PUMA ZACHANGIA KUFANIKISHA WIKI YA NENDA KWA USALAMA BARABARANI

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Pereira Ame Silima (kushoto)akipokea sehemu ya ya stika maalum kwa ajili ya kampeni ya usalama barabarani toka kwa wadhamini wa stika hizo kwa mwaka huu Airtel na Puma, wanaokabidhi  (kutoka kulia) ni  Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Bi. Beatrice Singano na Mkurugenzi wa kampuni ya Mafuta Puma Bw. Maregesi Manyama. Anayeshuhudia  ni Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, SACP Mohamed Mpinga. Airtel Tanzania na Puma ni wadhamini wakuu wa wiki ya uhamasisaji wa wiki ya Nenda kwa usalama ambapo mwaka huu kitaifa itafanyika mkoani Iringa ikiwa imebeba ujumbe usemao “ Pambana na ajiali za barabarani kwa vitendo, zingatia sheria. 

Kamanda Mpinga akionyesha jinsi ya kufungua na kubandika stika hizo maaalum.
*******************************
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel ikishirikiana na kampuni ya mafuta PUMA kwa pamoja wameungana na serikali ya jamuhuri ya Tanzania kwa kupitia baraza la taifa la  usalama barabarani na Jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani katika kuhakikisha elimu kuhusu usalama barabarani inatolewa ili kuthibiti idadi ya ajali za barabarani nchini.

Kutangazwa kwa ushirikiano huo kumefanyika leo katika ofisi za mkao makuu ya PUMA ambapo Mkuu wa kitengo cha usalama barabarani Tanzania Kamanda Mohamed Mpinga ametangaza wiki ya nenda kwa usalama barabarani ya mwaka huu itakayozinduliwa rasmi siku chache zijazo huko mkoani Iringa.

Akiongea wakati wa halfa hiyo mgeni rasmi , Naibu Waziri  wa mambo ya ndani Mheshimiwa Pereira Ame Silima alisema” nachukua fulsa hii kuwashukuru wadhamini wa kampeni ya usalama barabarani kwa mwaka huu kampuni ya simu za mkononi ya Airtel na  Kampuni ya Mafuta ya PUMA kwa kutoa mchango wao wa pamoja na kushirikiana na jeshi la polisi usalama barabarani kufikia malengo kwa kuhakikisha usalama wa raia na kupunguza ajali za barabarani ”

Ajali za barabarani zinaongezeka kwa kasi na kusababisha upotezaji wa nguvu kazi huku zikiacha maafa makubwa kwa taifa, ni jukumu la kila mtanzania kuwa sehemu ya kusimamia na kuzingatia sheria za barabarini  huku tukiishi na kutimiza kauli mbiu ya mwaka huu “Pambana na Ajali za barabarani kwa vitendo, Zingatia Sheria”.

Nachukua fulsa hii kuwaaasa watumiaji wa vyombo vya moto kupeleka magari yao kukaguliwa na kuthibitishwa ubora wa kutembea barabarani ili kuhakikisha vyombo vinavyotumika kubeba abiria viko salama na vinakidhi viwango vilivyowekwa kuhakikisha usalama barabarani.”  aliongeza Silima

Akiongea kwa niaba ya Airtel, Mkuu wa kitengo cha mawasiliano Beatrice Singano Mallya alisema “Airtel tunajivunia kuwa sehemu ya juhudi za kuokoa maisha ya watanzania  na mali zao na tunayo dhamira ya kuhakikisha tunashirikiana na wadau wote wenye wito wa kusaidia usalama barabarani  na jeshi la polisi usalama barabarani kupunguza ajali za barabarini kwani ushika hiuu wa Airtel leo ni moja kati ya shughuli za kijamii tunazozifanya nchini. 

Nia na madhumuni yetu makubwa ni kusaisdia sshughuli zinazofanywa na jeshi la polisi kusimamia na kupunguza maokeo ya ajali za barabarani, kila mwaka kuna kunakua na matukio ya ajali za barabarani ambazo zingeweza kuepukika kama wahusika wangekua na elimu ya kutosha. Hii ndio sababu kubwa na madhumini ya Airtel kuwa mmoja ya washiriki wakuu katika kusaidia kuhamasisha na kutoa elimu itakayofanikisha upungufu wa ajali barabarani kwa wa tano sasa.”.

Akizungumza kwa niaba ya kampuni ya mafuta ya PUMA ENERGY Mkurugenzi Mkuu wa PUMA ENERGY ndugu MAREGESI BEN MANYAMA… alisema “tuna malengo makuu matatu kuhusu usalama kazini nayo ni kutokua/kutosababisha ajali, kutoumiza mtu yeyote na kutoharibu mazingira. Sisi tunaamini kuwa Baraza la Usalama Barabarani lina jukumu kubwa na muhimu sana la kupunguza ajali za barabarani. Hivyo mchango wetu kusaidia juhudi za Baraza, zinaendana sawasawa na malengo yetu ya usalama. Kama huu msaada wetu mdogo utafanikisha kuepusha hata kifo kimoja, sisi tutaona kuwa malengo ya msaada yatakuwa yamefikiwa. PUMA ENERGY wamakuwa wabia wa muda mrefu (kabla ya hapo BP Tanzania) wa masuala ya Usalama Barabarani. Ni nia yetu kwamba tutaendelea kushirikiana na jeshi la Polisi pamoja na wadau wengine kuendelea na mapapambano ya kupunguza ajali nyingi ambazo tunaamini nyingi zinaweza kuzuilika”

Nae kamanda mkuu wa jeshi la usalama Tanzania afande Mohamed Mpinga alisema.”Tunatoa wito kwa watu wote kushirikiana nasi kufanikisha zoezi hili na nimatumaini yetu elimu tutakayoendelea kuitoa kwa wananchi itasaidia katika kupunguza na kudhibiti ajali zinazotoka barabarini nakusababisha maafa makubwa kwa taifa na jamii kwa ujumla. 

Tunawaomba watanzania wote wahakikishe magari yao yamefanyiwa ukaguzi katika kipindi hiki cha usalama barabarani na rai yetu sio tu kwa wakazi wa Iringa ila pia ni kwa watanzania wote katika mikoa yote nchini.

Airtel kwa mwaka huu imechangia  kuchapisha stika, kutoa elimu kwa kupitia vyombo za habari nchini pamoja  na kutoa vitu mbalimbali ikiwemo T shirt 800 zenye ujumbe  wa mwaka huu “Pambana na Ajali za barabarani kwa vitendo, Zingatia Sheria”. Tunaamini ajali za barabarani zinaweza kuepukika ikiwa kila moja atafanya sehemu yake Mallya aliongeza.

Airtel imekuwa mstari wa mbele katika kuchangia shughuli za usalama barabarani nchini , kwa miaka 4 mfululizo sasa Airtel kwa kushirikiana na Baraza la Usalama Barabarani imekuwa ikijitahidi kuhakikisha ajali zinadhibitiwa.

No comments: