Tangazo

September 13, 2012

MAMA SALMA ATEMBELEA VITUO VYA WATOTO YATIMA

 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea shada la maua kutoka kwa mtoto Agnes Wanjiru, 5, wakati alipowasiri kwenye kituo cha kulelea watoto wadogo cha Thomas Barnados mjini Nairobi tarehe 12.9.2012.



Mama Salma Kikwete akiwa katika kituo cha kulelea watoto wadogo cha Thomas Barnados aliweza kuwapakata, kuwabeba watoto mbalimbali wanaolelewa kituoni hapo.

Mama Salma Kikwete akiangalia kazi za wanafunzi wa chekechea wanaolelewa katika kituo cha Thomas Barnados kilichopo jijini Nairobi wakati alipotembelea shuleni hapo tarehe 12.9.20012.  Mama Salma ameambatana na Rais Kikwete kwenye ziara ya kiserikali nchini Kenya.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa mwanafunzi wa 'Starehe Girls Centre' waliokuwa katika maabara ya shule hiyo wakifanya practicals katika somo la kemia. Shule hiyo huchkua watoto wanafanya vizuri katika masomo ya msingi lakini hukosa uwezo wa kujiunga na sekondari.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiangalia bidhaa mbalimbali za ufinyanzi zinazotengenezwa na kiwanda cha Kazuri kilichoko Nairobi tarehe 12.9.2012. PICHA NA JOHN LUKUWI

No comments: