Tangazo

September 13, 2012

KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI CHATEMBELEA TBL

Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo (kushoto) akitoa maelezo mbele ya ujumbe wa Kikosi cha Polisi cha Usalama wa Barabarani, jinsi Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), inavyotoa inavyowatahadharisha watu kutolewa wakati wakiendesha vyombo vya moto. Ujumbe huo ulialikwa kutembelea Makao Makuu ya kampuni hiyo, jijini Dar es Salaam juzi.

Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Steve Kilindo (kulia), akitoa historia ya kampuni hiyo kwa ujumbe wa Kikosi cha Polisi cha Usalama wa Barabarani, uliotembelea kiwanda cha kampuni hiyo, Dar es Salaam.

Mnadhimu Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Johansen Kahatano (kushoto), akiipongeza Kampuni ya Bia Tanzania (TBL). kwa utaratibu waliowawekea madereva wa malori yao ikiwemo vidhithiti mwendo na muda mfupi wa kuendesha magari hayo hivyo kupunguza ajali. Kahatano aliongoza ujumbe wa askari 9 kutembelea kiwanda cha kampuni hiyo, Dar es Salaam.

Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Kuruthum Bambe akiuliza swali kwa uongozi wa TBL.

Meneja wa Usalama mahali pa Kazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Renatus Nyanda (katikati), akitoa maelezo jinsi mitambo ya kusafisha maji taka kuwa safi, wakati ujumbe wa askari 10 wa Kikosi cha Polisi cha Usalama wa Barabarani, ulipotembelea kampuni hiyo, Dar es Salaam juzi. Kulia ni kiongozi wa ujumbe huo Mnadhimu Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Johansen Kahatano. Kutoka kushoto ni, ASP Emilian Kamuhanda na Mkaguzi wa jeshi hilo, Theresia.

Meneja wa Usalama mahali pa Kazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Renatus Nyanda (katikati), akitoa maelezo jinsi mitambo ya kusafisha maji taka kuwa safi, wakati ujumbe wa askari 10 wa Kikosi cha Polisi cha Usalama wa Barabarani, ulipotembelea kampuni hiyo, Dar es Salaam juzi. Kulia ni kiongozi wa ujumbe huo Mnadhimu Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Johansen Kahatano. Kutoka kushoto ni, SSGT Enock Machunde, ASP Emilian Kamuhanda na Mkaguzi wa jeshi hilo, Theresia Kimaro.

Meneja wa Usalama mahali pa Kazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Renatus Nyanda (kushoto), akiuongoza ujumbe wa Kikosi cha Polisi cha Usalama wa Barabarani kutembelea eneo la upishi wa bia, wakati askari hao walipotembelea kiwanda cha kampuni hiyo, Dar es Salaam juzi. Kutoka kulia ni, SSGT Enock Machunde, ASP Emilian Kamuhanda na Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Kuruthum Bambe na Mnadhimu Mkuu wa Kikosi hicho, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Johansen Kahatano.

Mtaalam wa Upishi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Adolf Ndyeabura (kushoto) akitoa maelezo jinsi mitambo inavyochuja bia wakati ujumbe wa askari 10 wa Kikosi cha Polisi cha Usalama wa Barabarani, ulipotembelea kiwanda cha kampuni hiyo, Dar es Salaam juzi, ikiwa ni moja ya shamrashamra ya maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama.
Mtaalam wa Upishi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Adolf Ndyeabura (kulia) akitoa maelezo jinsi mitambo inavyochachusha bia wakati ujumbe wa askari 10 wa Kikosi cha Polisi cha Usalama wa Barabarani, ulipotembelea kiwanda cha kampuni hiyo, Dar es Salaam juzi, ikiwa ni shamrashamra ya maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama.

No comments: