Tangazo

September 13, 2012

WAZIRI WA UJENZI DK. JOHN MAGUFULI AKAGUA UJENZI WA DARAJA LA KIGAMBONI NA BARABARA YA KILWA

Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akijiridhisha kwa kupima kiwango cha lami inayowekwa upya katika barabara ya Kilwa na Kampuni ya Kajima ya Japan leo jijini Dar es salaam. Wengine wanaoshuhudia kutoka kulia ni mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki, Balozi wa Japani nchini Tanzania Masaki Okada na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Kajima.

Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli (mbele) akiwa amefuatana na balozi wa Japan nchini Tanzania Masaki Okada, Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam na viongozi wengine wa wizara akikagua moja ya sehemu ya barabara ya Kilwa inayojengwa upya na kampuni ya KAJIMA  ya Japan kutokana na barabara hiyo iliyokamilika hapo awali kuwa chini ya kiwango na serikali ya Tanzania kuikataa na kuiagiza kampuni hiyo iijenge upya kwa gharama zake.

Wafanyakazi wakiendelea na ujenzi wa barabara ya Kilwa leo jijini Dar es salaam.

Mhandisi mkazi wa Kampuni ya Kajima ya Japan inayojenga upya barabara ya Kilwa Hisashi Muto(kushoto) akitoa maelezo ya awali ya ujenzi wa barabara hiyo kwa Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli leo jijini Dar es salaam.

Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akikagua ujenzi wa daraja la Kigamboni akiwa ameambatana na viongozi wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Saidi Mecki Sadiki (wa pili kutoka kulia) Mbunge wa Kigamboni Dkt.Faustine Ndugalile (wa tatu kutoka kulia) leo jijini Dar es salaam. Daraja la Kigamboni linajengwa na kampuni ya China Railways Engineering kwa gharama ya shilingi bilioni 214 na linatarajia kukamilika kabla ya mwaka 2015.

Daraja la Kigamboni likiendelea kujengwa katika bahari ya Hindi eneo la Kurasini. Daraja hilo litakapokamilika litakua na njia 6 pamoja na barabara za juu na kuwa moja ya Daraja kubwa na la kipekee Afrika mashariki na kati. 

 Mmoja wa wafanyakazi wa daraja hilo ambaye jina lake halikupatikana mara moja akiendelea na zoezi la kupiga picha huku akiwa amesimama kwenye mtambo unaopitisha umeme mwingi bila kuchukua tahadhali wakati waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli alipokua akikagua maendeleo ya ujenzi wa  daraja hilo leo.Picha na Aron Msigwa -MAELEZO

No comments: