Tangazo

October 8, 2012

KAMPUNI YA GREEN WASTE PRO YALALAMIKIA UJENZI USIOFUATA TARATIBU KUCHAFUA MAZINGIRA YA MJI

Malori yanayobeba Udongo katika eneo hilo la Ujenzi yakiingia na kutoka wakati wa usiku huku yakiwa hayjafunikwa na maturubai hali inayosababisha kumwaga udongo katika barabara za jiji na kusababisha uchafuzi unaolalamikiwa na kampuni zinazofanya usafi.
Bango la Mkandarasi anayejenga jengo hilo lililopo kwenye kiwanja namba 01 katika makutano ya Barabara ya Ali Hassan Mwinyi na Ufukoni jijini Dar es Salaam ambapo linaonyesha Wajenzi ni Kampuni ya China Railway Jiachang Engineering Co. Ltd.
Moja ya Malori ya mchanga likitoka baada ya kuzoa udongo katika jengo hilo na kujazwa kupita kiasi.
Muonekano wa uchafu katika barabara kutokana na kumwagika kwa udongo unaozombwa na malori hayo ambao unapelekea kuzibisha mitaro na kuchakaza lami.
Malori yakiwa kwenye foleni ya kuzoa udongo katika jengo hilo.
Na Mwandishi Wetu

Tunapozungumzia Suala la usafi asilimia kubwa ya wanajamii wanaelewa maana yake na umuhimu wake.

Na tunapozungumzia kutunza usafi katika mazingira yetu tunamaanisha kuanzia tunapoishi hadi katika barabara za ndani na zile kubwa za lami zinazotumika mijini.

Wote tumeshuhudia Manispaa ya Ilala ambayo ndio kitovu cha jiji la Dar es Salaam ikizindua kampeni za kufanya usafi katika maeneo yote ikimo katika barabara kubwa za jijini.

Katika kutimiza malengo hayo kampuni ya ‘Green Waste Pro Ltd’ ikafanikiwa kushinda zabuni ya kufanya usafi katika manispaa hiyo.

Ama kwa hakika kapuni hiyo yenye magari yakutosha likiwemo gari la kisasa la kupiga deki barabarani ikaanza kazi hiyo na kipindi kifupi matokeo yakaaanza kuonekana.

Sasa basi katika kile kinachoonekana kama ama kutojali au kupuuzia taratibu za usafi kampuni moja iliyopewa kandarasi ya kujenga jengo moja katika ene la mtaa wa Ufukweni jiji Dar imekuwa ikichafua mazangira ya jiji bila kujali.

Mo Blog imeshuhudia magari makubwa ya kampuni hiyo yakibeba udongo nyakati za usiku huku yaendeshwa hovyo na kumwa udongo huo barabarani na kuacha vumbi likitimka hewani.

Tukizungumza na Mkurugenzi wa Kampuni ya ‘Gree Waste Pro Ltd’ Bw. Mac Antony Shayo amesema kwa kawaida magari yanayofanya shughuli hiyo yanapswa kusafishwa pale pale kwe saiti kabla ya kutoka nje, ili kuepuka kuchafua mji.

Ameongeza kusema kuwa kingine ni kwamba magari hayo yanajazwa sana udongo kuliko kiwango kinachoshauriwa na pia hayafunikwi, hivyo yanamwaka tu matope barabara yote kuanzia yanakotoka, na mbaya zaidi yanaingia ‘City Centre’.

Amesema kuwa utaratibu huo sio sahihi na gharama zinazotumika kusafisha barabara ni kubwa na kinachojitokeza kuwa sasa tunashinda sisi tunafiwa wao wanakazana kuchafua.

Bw. Shayo amesema pamoja na kuchafua barabara pia ndio chanzo cha uharibifu wa lami, na pia udongo kujaa katika mifereji kipindi cha mvua.

Aidha amesema kampuni hiyo inapaswa inyimwe kuendelea na kazi hiyo mpaka itakaporekebisha taratibu zao za utendaji ikiwemo kusafisha hayo magari yao ili yaweze kubeba uchafu kwa njia ya usafi.

Afafanua kuwa gari hizo zisijazwe na zifunikwe kama sheria inavyotaka kwa kuwa sheria haikuwekwa ili mtu asimamiwe bali imewekwa ili itekelezwe.

No comments: