Na Father Kidevu Blog, Dar Es
Salaam
KAMATI ya Miss Tanzania imesema
kuwa Mrembo Maggie Munthali hana pingamizi lolote katika kushiriki mashindano
hayo kwa kutumia jina la Tanzania na badalaye kufanya hivyo anatumia uzalendo
wake kuitangaza nchi Kimataifa.
Ufafanuzi huo umekuja kufuatia
malamiko yaliyotolewa na baadhi ya wadau wa Urembo hasa Watanzania waishio
katika jiji la Washingtoni DC, Marekani juu ya Uhali wa Mrembo Maggie Munthali
kuvaa beji ya Miss Tanzania katika mashindano ya kumsaka Miss Afrika USA 2012.
Akizungumza na Blogu hii Msemaji
wa Kamati ya Miss Tanzania Hidan Ricco amesema kuwa Kamati ya Miss Tanzania
haina kipingamizi chochote kwa mrembo huyo kushiriki mashindano hayo, kwani
shindano hilo linawahusu warembo waishio huko lakini wanatoka Tanzania.
Awali akitoa historia ya
Mrembo huyo, Rico alisema kuwa Kamati inamfahamu vyema mrembo Maggie Munthali
kwani aliwahi kushiriki mashindano hayo ngazi ya Vitongoji na kuishia ngazi ya
kanda.
Tumesoma maoni yenu kupitia
mitandao ya kijamii Blogs inaohusu taarifa ya mrembo Maggie Munthali kushiriki
shindano la urembo la Miss Africa USA.
“Mrembo Maggie Munthali alishiriki mashindano ya urembo ya Miss Tanzania Kitongoji cha MZIZIMA mwaka 2005.” Alisema Ricco.
Pia aliendelea kwa kusema kuwa
Mrembo Maggie alikuwa miongoni wa waliofanikiwa kuingia TOP 3 ya shindano hilo
hivyo kupata nafasi ya kuwakilisha kitongoji hicho katika ngazi ya KANDA YA
ILALA kwa mwaka huo.
Mrembo huyo hakupata nafasi ya kuingia katika Fainali za Taifa kwa mwaka huo 2005. aliishia ngazi ya Kanda ya Ilala.
Kanda ya Ilala kwa mwaka huo iliwakilishwa na FEZA KESSY, Perminda Raj na LILIAN MUSHI, na mshindi wa mwaka huo alikuwa NANCY SUMARI ambaye pia alitwaa taji la MISS WORLD AFRICA 2005.
Ricco amesema Kamati ya Miss Tanzania
haijui ni vigezo vipi vinatumika katika shindano hilo, na maamuzi yakumpa jina
Miss Tanzania na Kamati inaamini kuwa ni mrembo anayewakilisha Tanzania
japokuwa hakuingia katika Fainali za Taifa.
Kamati inamtakia kila la heri mrembo huyo na wengine watakaojitokeza kutangaza jina la Tanzania katika fani ya urembo.
Father
Kidevu Blog ilifanikiwa kufanya utafiti juu ya washiriki wa shindano
hilo na kubaini kuwa sio Mamiss halisi wa nchi walizotoka kwani baadhi
ya nchi walikuwa zaidi ya mmoja kama vile Kenya.
Pia baadhi
yao Umri unaonesha dhahiri kuwa umekwenda sana kwani washiriki
wanapoaswa kuana miaka kuanzia 18 lakini isizidi 29 na hawaendani na
vigezo halali vya mashindano ya Urembo yanayofanyika kila mwaka katika
nchi husika kwaajili ya kushiriki Miss World.
Haya ni baadhi ya Masharti na Vigezo vya Mshiriki ambayo yapo
katika mtandao huu http://www. missafricaunitedstates.com/ application/registration/
ELIGIBILITY
1.Applicant must have at least one parent from an African country.
2. An applicant with parents from two countries will choose to represent only one country of her choice.
3. Applicants must be at least 18 years old on or before the date of the pageant she wishes to compete in.
4.Applicants above 29 years of age will not be accepted
5.We accept Applications from students, professionals and girls wishing to develop themselves and improve their status.
6. Applicants are strongly encouraged to have a humanitarian platform and realistic project to uplift the community in need.
7. No Pageant Experience is required.
8. Applicants must be female at birth and never married.

No comments:
Post a Comment