Tangazo

March 18, 2013

Askari Trafiki agongwa na gari Bamaga -Dar



Askari wa kike wa Kikosi cha Usalama Barabarani aliyejulikana kwa jina moja la Elikiza aliyekuwa akiongoza magari eneo la Bamaga, Mwenge jijini Dar es Salaam, akifunikwa na wasamaria wema baada ya kugongwa na gari na inadhaniwa kuwa amekufa papo hapo.Picha na Shauri Kati / GPL
--
Trafiki mmoja ambaye amefahamika kwa jina moja la Elikiza, majira ya mchana amegongwa na gari aina ya VX ambayo haikujulikana namba na inadhaniwa kuwa amekufa papo hapo wakati akiongoza magari eneo la mataa ya Bamaga, Mwenge jijini Dar es Salaam.

Taarifa zilizopatikana eneo la tukio zinadai kuwa Trafiki huyo alikuwa akiongoza msafara na baada ya msafara huo, aliruhusu magari mengine yaendelee na safari ndipo ghafla gari lilipotoka upande wa pili na kumgonga.

No comments: