Tangazo

March 20, 2013

Zijue tabia 30 zinazoashiria umezeeka: Kama ukiona moja wapo unayo basi ujue ni saa kumi na moja na nusu anza kuaga

1. Huna muda wa kushinda na mp...enzi wako kutwa nzima mkipiga stori za mapenzi

2. Ukihitaji kufanya mapenzi mahali unakokufikiria ni kitandani

3. Unaanza kujaza friji lako kwa vyakula zaidi kuliko pombe

4. Muziki unaoupenda unausikia ukiwa kwenye lifti ama kwenye gari lako ukienda na kutoka kazini

5. Saa 11 alfajiri ndiyo muda unaoamka, na siyo muda tena unaorudi kulala

6. Unatazama taarifa ya habari hadi utabiri wa hali ya hewa

7. Rafiki zako wanakualika zaidi kwenye vikao vya harusi kuliko mtoko wa kwenda Maisha Club

8. Ukienda dukani kununua kitu unakuwa na juhudi sana ya kuomba upunguziwe bei

9. Idadi ya t-shirt na jeans inapungua kwa kasi kwenye kabati lako la nguo

10. Wewe ndiyo unayekumbuka kuwapigia simu Polisi endapo mtaani kwenu kuna vijana wavuta bangi wanaowasumbua

11. Ndugu zako watu wazima wanajisikia kawaida tu kufanya utani wa kiutu uzima mbele yako

12. Hukumbuki tena Azam Ice Cream na Samaki Samaki wanafunga saa ngapi

13. Timu yako ya mpira ikifungwa hutaki tena kutaniwa na watu

14. Wanyama uwapendao kama mbwa na paka unawaandalia chakula kwa kanuni za kisayansi badala ya kuwalisha makombo

15. Ukilala kwenye kochi unaamka mgongo unakuuma sana

16. Unaithamini sana ratiba yako ya kulala

17. Ukiwa nyumbani unaanza kutumia muda wako wa ziada kulimalima bustani ya maua ama mbogamboga badala ya kutazama filamu na kuzurura

18. Kila kitu kikinunuliwa nyumbani jambo la kwanza unalouliza, "Umenunua sh. ngapi?"

19. Unakwenda duka la madawa kununua Ibuprofen na Antacid, siyo kondomu tena wala kipima mimba

20. Unaanza kununua magazeti ya Mwananchi, The Guardian, Daily News, Citizen na Nipashe badala ya Uwazi, Ijumaa, Kiu na Amani

21. Unapata kifungua kinywa kwa wakati

22. Ukiwa baa unanunua bia unazohitaji wewe badala ya kusema "zungusha kama tulivyo"

23. Asilimia 90 ya muda unaoutumia kwenye kompyuta yako unautumia kufanya kazi badala ya kuchati

24. Ukijisikia hamu ya kunywa kilevi unaanza kunywea nyumbani ili kupunguza gharama kabla hujaenda baa

25. Ukimwona rafiki yako ana ujauzito unampongeza sana badala ya kumwuliza, "imekuwaje tena?"

26. Ukienda kutembea mahali unaulizia bei za viwanja

27. Hupendi tena kuwaazimisha marafiki zako magari yako

28. Ukiwa na rafiki zako unapenda kujadiliana nao kuhusiana na mfumuko wa bei, na mfumo mbovu wa utawala

29. Ukiwa unakula chakula unakuwa mkali ikitokea chakula kimewekwa mafuta mengi ama chumvi nyingi

30. Kwa wanawake utaanza kuona vijana wanakukimbia na kwa wanaume utaanza kuona vibinti vinakupapatikia sana.

Chanzo: Facebook

No comments: