Tangazo

May 29, 2013

AIRTEL YAZINDUA MICHUANO YA AIRTEL RISING STARS 2013

Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano Mallya akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa progam ya Airtel Rising Stars 2013 uliofanyika katika Ofisi za TFF jijini Dar es Salaam, wengine ni Mkurugenzi wa Michezo Leonard Thadeo(katikati) na Makamu wa Raisi wa TFF Ramadhani Nasibu.

Baadhi ya wachezaji wa Airtel Rising stars wa mwaka 2012 wakisalimiana na Mkurugenzi wa Michezo Leonard Thadeo, Makamu wa Raisi wa TFF Ramadhani Nasibu na Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano Mallya wakati wa uzinduzi wa progam ya Airtel Rising Stars 2013 uliofanyika katika Ofisi za TFF jijini Dar es Salaam.

Wakizindua program ya Airtel Rising Stars 2013 Mkurugenzi wa Michezo Leonard Thadeo, Makamu wa Raisi wa TFF Ramadhani Nasibu na Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Tanzania Beatrice Singano Mallya, Kaimu katibu mkuu wa TFF Sunday Kayuni na mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu Dar es Saalam Almasi Kasongo wakati wa uzinduzi wa Airtel Rising Stars 2013.

No comments: