Tangazo

May 20, 2013

Kampeni ya Afya ya Mama na Mtoto nchini; Montage yakabidhi Milioni 70/- kwa WAMA

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea mfano wa hundi ya shs 70 milioni kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Montage Bibi Teddy Mapunda ikiwa ni sehemu ya michango iliyokusanywa wakati  wa harambee iliyofanyika katika hoteli ya Serena hapa Dar kwa ajili ya afya ya mama na mtoto hapa nchini. Wengine katika picha (L to R) Ni Ndugu Mwanahamisi Kitogo, Msaidizi wa Mama Salma, Ndugu Beatrice Mkindi, Mkurugenzi wa Fedha wa Montage, Ndugu Joyce Mhavile, Mkurugenzi  Mtendaji  wa  ITV na wa mwisho ni Ndugu Daud Nassib, Katibu wa WAMA.

Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete akitoa neno la shukrani kwa uongozi wa Montage mara baada ya kupokea hundi ya shs 70 milioni iliyopatikana wakati wa harambee ya kuchangia afya ya mama na mtoto iliyofanyika katika hoteli ya Serena hapa Dar hivi karibuni.

Mwenyekiti wa WAMA na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wakuu wa Montage na wale wa WAMA mara baada ya kupokea hundi ya shs 70 milioni kwa ajili ya afya ya mama na mtoto.

Mama Salma Kikwete akiagana na Mkurugenzi wa Montage Bibi Teddy Mapunda mara baada ya makabidhiano ya hundi kwa ajili ya afya ya mama na mtoto iliyofanyika katika ofisi za WAMA. PICHA NA JOHN LUKUWI

No comments: