Tangazo

May 16, 2013

Mamlaka ya udhibiti na usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) pamoja na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii yaendelea kutoa elimu kwa waheshimiwa wabunge pamoja na waandishi wa habari katika maonesho ya wiki ya hifadhi ya jamii mjini Dodoma

 Waziri wa Kazi na Ajira Mhe. Gaudentia Kabaka akifungua rasmi semina ya waandishi wa habari iliyoandaliwa na SSRA na Mifuko ya Hifadhi ya jamii.
  Mkurugenzi Mkuu wa SSRA Bi Irene Isaka akijibu baadhi ya maswali ya waandishi wa habari. Pembeni yake ni waziri wa kazi na ajira Bi Gaudentia Kabaka pamoja na naibu waziri Dr Milton Makongoro Mahanga
 Mmoja wa waandishi wa habari akichangia mada katika semina ya waandishi wa habari.
 Mkurugenzi Mkuu wa SSRA Bi Irene Isaka akiwasilisha mada kuhusu sekta ya hifadhi ya jamii kwa waheshimiwa wabunge. 
Mkurugenzi Mkuu wa GEPF Bw Daud Msangi akiwasilisha mada juu ya mchango wa GEPF katika kuendeleza sekta ya hifadhi ya jamii.
 Mhe Juma Nkamia akishiriki katika mada.
Naibu Spika Mh Job Ndugai akifungua rasmi semina maalum ya waheshimiwa wabunge iliyoandaliwa na SSRA na Mifuko ya Hifadhi ya jamii mjini Dodoma.

Mh. Anna Abdallah akiuliza swali juu ya shughuli za Mifuko ya Hifadhi ya jamii.

No comments: