Tangazo

May 30, 2013

WADAU WA TCAA WAKUTANA DAR

Mkurugenzi Mtendaji kutoka  Equity Aviation Services (T) Ltd Rosemary Kacungira  akichangia mkutano wa wazi wa  maboresho ya utoaji wa leseni kwa makampuni  katika mkutano wa siku moja wa wadau wa sekta ya usafiri salama wa anga  jijini Dar es Salaam Mei.29.2013. PICHA/MWANAKOMBO JUMAA WA MAELEZO

Mwenyekiti wa  Baraza la watumiaji wa huduma za usafiri wa anga Tanzania  Juma Fimbo(kulia)  na Katibu  Mtendaji wake Hamza Johari wakitoka baada ya kumalizika kwa kikao kilichowakutanisha wadau wa anga  Mei 29.2013 jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa  Mamlaka ya Usafiri wa Anga Fadhili Manongi (kulia) akizungumza wakati wa mkutano huo  wa wazi wa siku moja wa maboresho ya utoaji wa leseni  kwa makampuni mbalimbali yanayohudumia viwanja vya ndege nchini. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya TCAA , Juma Mbwana Juma.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Alia Aviation Consultants Mahmud .M. Shamte (aliesimama) akifafanua jambo katika mkutano huo wa maboresho ya utoaji wa leseni  kwa makampuni yanayohudumia viwanja vya ndege . Mei 30.2013 jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wadau wa mkutano wa wazi wa maboresho wa utoaji wa leseni kwa makampuni yanayohudumia viwanja vya ndege nchini wakifuatilia mada mbalimbali katika mkutano wa siku moja  uliofanyika  Mei 29.2013, jijini Dar es Salaam ulioandaliwa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Mkutano huo umezungumzia masuala mbalimbali  jinsi ya kuboresha huduma za usafiri wa  anga pamoja na changamoto  mbalimbali zinazowakabili wadau wa sekta hiyo.

No comments: