Tangazo

May 13, 2013

Wafanyakazi 56 wa Airtel Tanzania watunukiwa Tuzo

 Mkurugezi wa mauzo na masoko  wa Airtel bw  Mustafa Kapasi (kushoto) akimkabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo  Afisa mauzo kanda ya dar es salaam  Airtel  John Gondwe  baada ya kuhitimu mafunzo ya mauzo na usambazaji ya muda wa miaka miwili yanayoendeshwa na Airtel Centum Sales University (ACSU). Wafanyakazi 56 kutoka katika mikoa mbalimbali walihitimu mafunzo hayo, akishuhudia katikati ni Mkurugenzi Rasilimali watu Patrick Foya akifatiwa na Melvin Joel Meneja wa Centum Learning Makao Makuu.

 Meneja Mauzo wa Airtel Bw Stratory Mushi (katikati) akiwa katika picha ya pomoja na wahitimu mafunzo ya mauzo na usambazaji yanayoendeshwa na Airtel Centum Sales University (ACSU) wakati wa tafrija iliyofanyika katika ofisi za Airtel makao makuu morocco. Wahitimu hao ni wafanyakazi wa Airtel Tanzania.
Wahitimu mafunzo ya mauzo na usambazaji yanayoendeshwa na Airtel Centum Sales University (ACSU) wakikata keki kwa pamoja wakati wa tafrija iliyofanyika katika ofisi za Airtel makao makuu Morocco. Wahitimu hao ni wafanyakazi wa Airtel Tanzania.

Mkurugenzi wa Airtel, Bw. Sunil Colaso akiongea na wahitimu mafunzo ya mauzo na usambazaji yanayoendeshwa na Airtel Centum Sales University (ACSU) wakati wa tafrija iliyofanyika katika ofisi za Airtel makao makuu morocco. Wahitimu hao ni wafanyakazi wa Airtel Tanzania.

*****  *******
Airtel Tanzania, mtandao wa mawasiliano wenye gharama nafuu nchini leo imewakabidhi shahada wafanyakazi wake 56 waliohitimu mafunzo ya mauzo ya muda wa miaka miwili yanayoendesha na Airtel Centum Sales University (ACSU).

chuo cha masoko cha Airtel Centum Sales University kilizinduliwa Tanzania mwaka 2011, lengo la kuwaanda na kuwawezesha wafanyakazi wa Mauzo na usambazaji kupata ujuzi bora, elimu ya mauzo na usambazaji  utakaowawezesha kufanya kazi kwa ufanisi zaidi na kuhakikisha wauzaji wa rejareja wanaongeza ufanisi na kuongeza tija .

Akiongea katika halfa ya mahafali ya wahitimu hao yaliyofanyika katika makao makuu ya Airtel Moroco,Mkurugenzi wa Airtel Tanzania bwana Sunil Colaso alisema,” Programu hii ya Airtel Sales Academy inatolewa na Taasisi ya ukufunzi ijulikanayo kama Centum learning inayotoa mafunzo ya mauzo na usambazaji na kuwawezesha wafanyakazi wa Airtel kuwa bora zaidi Tanzania na Afrika kwa ujumla. 

Tunawapongeza wafanyakazi wetu kwa kazi nzuri waliofanya katika kipindi chote cha mafunzo yao na  tunaamini kwamba  mafunzo waliyopata  ya masoko na usambazaji yataleta mabadiliko na kuwapa wateja wetu huduma bora na zenye viwango vya juu ambazo hazijawahi kupatikana Tanzania.

Airtel tunaamini mikakati na malengo tuliojiwekea haitakuwa na tija bila kuwa na wafanyakazi wenye vipaji, wenye hari na nguvu watakao tumika kama vyombo muhimu kufanya ndoto na mipango yetu kuwa ya hakika aliongeza Colaso.

Airtel tunamini wafanyakazi ndio nguzo muhimu katika kuleta mabadiliko ya kitamaduni , kasi ya kazi na kibiashara.  kampuni imewekeza katika kukuza uwezo wa wafanyakazi na kutoa nafasi ya kukuza fani zao ndani ya kampuni. Mafunzo ya ujuzi daima imekuwa ni mikakati yetu inayoendana sambamba na ujuzi unaohitajika kimataifa.

Mafunzo ya ACSU yalianzishwa India mwaka 2009 yakiwa na lengo la kuongeza ujuzi, maarifa na ufanisi  endelevu kwa  wafanyaka  wa mauzo. Mpaka sasa zaidi ya wafanyakazi 80,000 wa vitengo mbalimbali wamepata mafunzo hayo.

Taasis ya Centum Learning inamilikiwa na Bharti na inatoa mafunzo yanayosaidia kuongeza ujuzi na kuleta ufanisi katika nchi  17 zikiwemo Africa, India, Bangladesh and Sri-Lanka.

Kwa maelezo zaidi kuhusu Centum Learning tembelea www.centumlearning.com

No comments: