Tangazo

August 21, 2013

WANYARWANDA WAZIDI KUTAPATAPA NA KUPIKA HABARI ZA UWONGO KWA UONGOZI WA TANZANIA, RAIS KAGAME APOPOLEWA KWA MAWE UINGEREZA


Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO  Bw. Assah Mwambene leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara hiyo amekanusha taarifa zilizoandikwa kwenye mtandao wa News for Rwanda na  wanyarwanda kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ni shemeji wa aliyekuwa Rais wa Rwanda Juvenal Havyarimana.

“Taarifa hizi haina ukweli wowote na zinalenga kumpaka matope Rais Jakaya Mrisho Kikwete,”amesema Mwambene na kufafanua kuwa lengo la mitandao ya kijamii ni kuhabarisha na kuelimisha umma wala siyo kupotosha jamii kwa kuandika habari zisizo na ukweli wowote.
Madai  hayo  yaliandikwa  jana  na  mitandao  ya  Rwanda  wakidai  kuwa  mama  Salma  Kikwete  ni  Mnyarwanda  na  ni  binamu  wa  aliyekuwa  rais  wa  zamani  wa  Rwanda. 
Wakati huo huo, wadadisi wa mambo wa kimataifa wameonesha kushangazwa na hatua ya makusidi ya Wanyarwanda ya kujaribu kumpakazia Rais Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete, Mmakonde  wa Lindi, kwa kumzushia mambo ya ajabu na kushangaa zaidi kuona mitandao hiyo ya udaku ya Rwanda haijaonesha jinsi Rais Kagame alivyovurumishiwa mawe na Wanyarwanda wenzake alipokuwa Chuo Kikuu ya Oxford nchini Uingereza.

"Unajua ustaarabu wa Watanzania ni wa hali ya juu ndio maana mitandao yake iliamua kuacha kuripoti habari za kutukanwa na kupigwa mawe Rais Kagame na Wanyarwanda wenzake wanaomchukia (angalia video) alipotembelea Chuo Kikuu cha Oxford hivi karibuni", amesema mdadisi mmoja  wa Uingereza, James Parker wa North London.

Mdadisi mwingine wa Uingereza, Bw. Mark Sutton, amesema hiyo ni moja ya njia chafu za Wanyarwanda katika kujaribu kulipiza kisasi kwa kutimuliwa maelfu ya ndugu zao waliokuwa wakiishi kinyume cha sheria nchini Tanzania, na sasa wanahaha wapi kwa kuwaweka kwenye ka-nchi hako kadogo ka Afrika Mashariki.
"Kutimuliwa kwa Wanyarwanda nchini Tanzania kutaleta vituko vingi sana, na hii ya kumsingizia Mama Salma Kikwete kuwa anahusiana nao ni mojawapo - mengi yatakuja na Watanzania wasishangae maana Wanyarwanda wametaharuki na hawajui wafanyeje kwa kupokea zaidi ya wenzao 10,000 waliokuwa wakiishi kinyume cha sheria nchini Tanzania," amesema mdadisi mwingine, Adam Hayes.

No comments: