Tangazo

August 19, 2013

Mwakilishi wa Big Brother The Chase, Feza Kessy akaribishwa kwa kishindo Nyumbani Lounge

Msanii maarufu nchini, Lady Jay dee maarufu 'Anaconda' akitumbuiza na bendi yake ya machozi bendi katika hafla ya kumkaribisha aliyekuwa mwakilishi wa Big brother wa The chase kutoka Tanzania, Feza Kessy.Hafla iliyofanyika maeneo ya nyumbani Lounge kwa udhamini mkubwa kabisa wa Airtel na DSTV.
Aliyekuwa mshiriki wa Big brother wa The chase kutoka Tanzania, Feza Kessy akisalimiana na mashabiki wake waliojitokeza katika halfa ya kumkaribisha   nyumbani iliyofanyika Nyumbani Lounge.
Aliyekuwa mshiriki wa Big brother wa The chase kutoka Tanzania, Feza Kessy (kulia), akiwa pamoja na Vanesa Mdee  wakati wa hafla ya kumkaribisha nyumbani iliyofanyika katika ukumbi wa nyumbani lounge na kudhaminiwa na DSTV na Airtel.
Msanii maarufu wa kundi la Machozi Band, Lady Jay dee akimtambulisha Feza Kessy kwa washibiki wake. 

No comments: