Tangazo

August 19, 2013

RAIS KIKWETE AMFARIJI MZEE PHILIP MANGULA KWA KUFIWA NA BINTI YAKE

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Mhe Philip Mangula kwa kufiwa na binti yake, Nemela Mangula, aliyefariki mwishoni mwa juma kwa ajali ya gari. Hapa ni nyumbani kwa Mzee Mangula Oysterbay jijini Dar es salaam leo Agosti 19, 2013.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Profesa Mark Mwandosya alipoenda kumfariji  Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Mhe Philip Mangula kwa kufiwa na binti yake, Nemela Mangula, aliyefariki mwishoni mwa juma kwa ajali ya gari. Hapa ni nyumbani kwa Mzee Mangula Oyterbay jijini Dar es salaam leo Agosti 19, 2013.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka sahihi kitabu cha maombolezo alipoenda kumfariji  Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Mhe Philip Mangula kwa kufiwa na binti yake, Nemela Mangula, aliyefariki mwishoni mwa juma kwa ajali ya gari.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpa mkono wa pole Mama Mangula. Kulia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Anne Makinda.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Mhe Philip Mangula na familia yake kwa kufiwa na binti yake, Nemela Mangula, aliyefariki mwishoni mwa juma kwa ajali ya gari. Anayefuata ni Profesa Mark Mwandosya, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Jordan Rugimbana na Bw. Ali Kikwete.


No comments: