Tangazo

December 11, 2013

Jaji Lubuva: Tume ya Uchaguzi iko huru

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC)  Jaji Mstaafu  Damian Libuva (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano wa NEC jijini Dares Salaam kuhusu tume hiyo iko huru. Kulia ni Mkurugenzi wa NEC,Julias Malaba.picha na Magreth Kinabo - Maelezo
Na Magreth Kinabo

 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC)  Jaji Mstaafu Damian Libuva ametoa  ufafanuzi kuwa tume  hiyo iko huru  na si kweli kwamba  haiko huru  kama inavyonukuliwa katika  baadhi ya taarifa na watu.

Kauli hiyo imetolewa leo na Jaji Lubuva wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano wa NEC jijini Dares Salaam, alisema  tume hiyo iliundwa kwa mujibu wa sheria kupitia Iba
 Jaji Libuva alisema kwa muda mrefu  katika chaguzi mbalimbali  yamekuwepo mlalamiko dhidi ya tume kuwa si huru  na  moja ya sababu zinazotolewa ni kutokana na mfumo wa uteuzi wa makamishina wa tume kuchaguliwa na Rais, ambaye ni  kiongozi wa Chama tawala.

“ Hili linapigiwa kelele hasa na vyama vya siasa na wadau wengine wa uchaguzi. Mara kadhaa katika mijadala limerudiwa rudiwa na hata baadhi ya vyombo vya habari vimenukuliwa vikisema hata Mwenyekiti wa Tume   ya Taifa ya Uchaguzi amekiri  kuwa tume siyo huru.

Tume inafanya kazi zake za kusimamamia na kuongoza shughuli za uchaguzi kwa uhuru ,na wazi bila kuingiliwa na chombo chochote iwe ni seriklai au  Chama chochote cha siasa,” alisema Jaji Lubuva.
Aliongeza kuwa  tume hiyo haijawahi kuagizwa kuendesha uchaguzi kwa kupendelea chama au mgombea yeyote.
 Aidha alisema katika mihadahra ambayo tume hiyo ilialikwa msimamo wa umekuwa ukitolewa  ni Tume  Huru. “ Nimetoa mada katika vyuo vikuu Iringa na Dares Salaam ambapo uhuru wa Tume umehojiwa katika mada hizo nimesisitiza juu ya suala hilo,” alisisitiza .

Jaji Lubuva alifafanua kuwa kwa vile mfumo uliopo wa tume hiyo ni wa Kikatiba, kama wananchi na wadau kwa ujumla wanataka mfumo wa uteuzi wa wajumbe wa tume ubadilike , basi wachukue fursa hiyo kutoa maoni yao kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba

No comments: