Tangazo

December 4, 2013

Rais Kikwete amteua Dr. Asha Rose Migiro kuwa Mbunge

DAR ES SALAAM, Tanzania
Rais, Dk. Jakaya Kikwete amemteua Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Maifa (UN) Mstaafu, Dk. Asha-Rose Migiro kuwa Mbunge.

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu Jijini Dar es Salaam, imesema, Uteuzi huo ambao umetangazwa na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi, ulianza tangu jana, Desemba 2, 2013.

Dk. Asha-Rose Migiro kwa sasa ni Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, anayesimamia Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI).

No comments: