Meneja Mradi wa Asasi ya Kijamii ya The Open Society Initiative For Eastern African Tanzania (OSIEA), Agnes Hanti akiongea wakati wa mafunzo kwa wadau wa Habari nchini juu ya changamoto zinazowakabili waandishi wa habari hasa katika haki ya kukuza demokrasia kwa waandishi wa habari yaliyofanyika leo Aprili 2, 2014 jijini Dar es Salaam.
Meneja Mradi wa Asasi ya Kijamii ya The Open Society Initiative For Eastern African Tanzania (OSIEA), Agnes Hanti akiongea wakati wa mafunzo kwa wadau wa Habari nchini (hawapo pichani) juu ya changamoto zinazowakabili waandishi wa habari hasa katika haki ya kukuza demokrasia iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Pembeni ni Mkurugenzi Msaidizi wa OSIEA, Mburu Gitu (Kulia).
Meneja Mradi wa Asasi ya Kijamii ya The Open Society Initiative For Eastern African Tanzania (OSIEA), Agnes Hanti akiongea na waandishi wa habari wakati wa majadiliano.
Waandishi wa Habari na wadau wa Habari nchini wakijadili juu ya changamoto zinazowakabili katika haki ya kukuza demokrasia iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Chuo Cha Uandishi wa Habari za Kibiashara (EABMTI), Bi. Rosemary Mwakitwange akifafanua changamoto mbali mbali zinazowakabili wanahabari mara baada ya kumalizika kwa mafunzo hayo.
Waandishi wa Habari na wadau wa Habari nchini wakijadili juu ya changamoto zinazowakabili katika haki ya kukuza demokrasia iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Waandishi wa Habari na wadau wa Habari nchini wakijadili juu ya changamoto zinazowakabili katika haki ya kukuza demokrasia iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
---
Asasi isiyo kuwa ya kiserikali ya OSIEA imesema kazikubwa inahitajika kufanyika ili kulinda Uhuru wa kujieleza na kujitegemea kwa vyombo vya habari nchini Tanzania. Wito huo unatokana na kuongezeka kwa vitendo vya kufungia vyombo vya habari na kuongezeka kwa matukio ya kuwadhuru waandishi wa habari pamoja na kuingiliwa kwa Uhuru wa wahariri na wanasiasa na wafanyabiashara.
Mwaka jana serikali ili yafungia magazeti binafsi ya Mwananchi na Mtanzania kwa siku 14 na 90 kwa tuhuma za kuchapisha habari zenye uchochezi ambazo serikali ilidai zinahatarisha usalama wa taifa na zinatishia uvunjifu wa amani na umoja.Gazeti jingine la Mwanahalisi liliamriwa kufungwa tangu mwezi Julai2012 na halijafunguliwa mpaka sasa. Sheria ya magazeti inaipa serikali mamlaka makubwa ya kukandamiza vyombo vya habari. Hatua zote hizo zinakwenda kinyume na sheria za nchi na haki za binadamu ambazo Tanzania imeridhia.
Pamoja ukweli kuwa vyombo vya habari binafsi vinaongezeka tangia mwaka 1990 lakini Uhuru wa wahariri wa vyombo hivyo bado una maswali mengi kuhusiana na baadhi ya vyombo kutumika kutanga biashara na kuwasaida wengine kisiasa. OSIEA inaitaka serikali na vyombo vya usalama kuheshimu Uhuru wa kujieleza na kutoa maoni na kuacha kuwanyanyasa waandishi wa habari. Waandishi wa habari lazima waweze kuzungumza na kuandika bila ya kuwepo kwa vizuizi vyovyote. OSIEA pia inaitaka serikali kuwasilisha Bungeni muswaada wa sheria ya vyombo vya habari ambao utaweka mazingira bora ya Uhuru wa vyombo vya habari.
Wakati Tanzania ikiwa katika maandalizi ya kupata katiba mpya, tunahitaji kukumbuka kuwa Uhuru wa vyombo vya habari na Uhuru wa kujieleza kwa waandishi wa habari ni kitu cha muhimu kwa ajili ya kusambaza taarifa kwa jamii. Sio tu haki ya jamii kupokea taarifa bali bila kuwa na Uhuru haitakuwa na maana yoyote kwa serikali yao. Uwezo wa kupata taarifa utawezesha kukua kwa demokrasia, kuongeza msisismko wa mijadala ya kitaifa kutoa taarifa zitakazoongeza uwajibikaji. Uhuru wa kupata habari una mchango mkubwa katika mchakato wa kupata Katiba mpya.
Licha ya kwamba Tanzania inakuza uchumi wake wa wakati lakini kusahau Uhuru wa vyombo vya habari kunaweza kukapunguza ufanisi wa ukuaji wa uchumi. Vyombo vya habari huru vinaweza kukuza kuimarisha jamii na kuvutia wawekezaji.
No comments:
Post a Comment