Na Magreth Kinabo –
MAELEZO
Mkuu wa Mkoa wa
Dar Es Salaam, Said Meck Sadiki (Pichani), amewataka wananchi wa mkoa huo wanapohisi wana
dalili za ugonjwa wa dengue kuwenda katika hospitali za Serikali kwa kuwa
matibabu hutolewa bila malipo.
Kauli hiyo
imetolewa na Mkuu huyo wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya
kuulizwa swali juu ya gharama kubwa za matibabu ya ugonjwa huo,
kwenye ukumbi wa mkutano wa Mwalimu J.K. Nyerere jijini Dares Salaam.
“Tunaomba wananchi
wanapohiisi dalili za ugonjwa huo kwenda katika hospitali za Serikali ,ambazo
ni Amana, Mwananyamala na Temeke kwa kuwa matibabu yanatolewa bila malipo”
alisema Sadiki.
Akizungumza na
mwandishi wa habari hizi,leo Msemaji wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,
Nsachris Mwamwaja alisema vituo vyote vya Serikali vinapaswa kutoa
matibabu ya ugonjwa huo bila malipo kwa kuwa ugonjwa huo ni mlipuko na
magonjwa ya milipuko matibabu yake hutolewa bila malipo.
Mwamwaja pia
alisema ikitokea hata vituo vya afya vya binafsi vikapewa vitenganishi na
vifaaa vya tiba na Serikali navyo vinasapwa kutoa matibabu ya ugonjwa huo bila
malipo.
Mkuu huyo wa mkoa
alisema kwa sasa wanajenga uwezo ili kila wilaya iwe na vituo vitano kwa
ajili ya matibabu ya ugonjwa huo.
Sadick aliongeza
kuwa Serikali itanyunyuzia dawa ya (Lavacide) sehemu za mikusanyiko kama vile
mashulenina kwenye madimbwi, lakini maeneo ya hotelini na mabaa watapaswa
kunyunyuzia dawa kwa gharama zao.
“ Kwa upande wa wizara,
idara na taasisi za Serikali wanapaswa kunyunyuzia dawa kwa gharama
zao,(yaani matumizi mengineyo)” alisisitiza huku akisema hata kwenye ofisi yake
wamefanya hivyo kwa gharama zao.
Aidha Sadiki aliwataka
viongozi wa mitaa na watendaji wengine kuwahimiza wananchi kuhusu usafi wa
mazingira ili kupunguza maambukizi ya ugonjwa huo.
Alisema wananchi
wanapaswa kuhakikisha vifuu vya nazi visoda kwani maji kidogo yanayokaa katika
vitu husababisha mbu wanaosabbaisha ugonjwa huo kuzaliana , hivyo
vinatakiwa visitupwe ovyo na kufunika maji safi wanayoyahifadhi.
Alisisitiza hatua
ya kwanza kuzuia ugonjwa huo ni usafi wa mazingira,hivyo dawa ni hatua ya
mwisho.
No comments:
Post a Comment