Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, Maisha
Maganga akiongea wakati wa uzinduzi wa duka la Airtel l lililopo maeneo ya
stendi ya Msamvu mkoani Morogoro ambapo Airtel pia ilitangaa rasmi maduka 15
mapya ambayo yanatoa huduma katika maeneo mbalimbali mkoani hapo.
XXXXXXXXXXXX
Morogoro,
KUFUATI
kutangaza mpango wake wa kuzindua maduka zaidi ya 2000 nchi nzima,
kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imezindua maduka 15 katika mkoa wa
morogoro kwa lengo la kuhakikisha bidhaa na huduma zake zinawafikia
wateja wake kwa ukaribu na urahisi zaidi
Akiongea wakati wa
uzinduzi , Meneja Mauzo kanda ya Morogoro, Albert Mtalemwa alisema “ leo
tunazindua maduka 15 mojawapo likiwa hapa ndani ya kituo cha mabasi kilichopo
Msavu Morogoro kwa lengo la kuwawezesha wasafiri na wale
wanaoingia kutoka maeneo mbalimbali, wafanyabiashara na wakazi wa Morogoro
wanaotembelea kituo hiki kupata huduma zetu za Airtel husasani huduma ya kifedha
kupitia simu za mkononi kwa urahisi zaidi na wakati wowote.
Maduka mengi ya Airtel
ambayo yanafanya kazi ya kutoa huduma yapo katika maeneo mbalimbali ambayo ni
pamoja na Itigi, Gairo,Kilombero na,mjini, Kilosa karibu na kituo cha mabasi,
Kimamba mjini, Ruaha, Dumila, Dakawa karibu na soko, Mikese karibu na
mizani, kituo cha Kisaki, Soko la Bwawani, Ifakara mjini
na Ifakara kituo cha basi.
Lengo letu ni
kuziweka huduma zetu karibu na wateja wetu ili kutatua changamoto zao za
mawasiliano kwa wakati na kuwawezesha kupata huduma za kifedha kwa urahisi.
Tunaamini maduka haya yataongeza idadi ya vituo vyetu na kuboresha kiwango
katika huduma zetu”. aliongeza Mtalemwa
Kwa upande wake Kaimu
Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, , Maisha Maganga alisema” nawapongeza
sana Airtel kwa mpango huu unaochochea kuboresha huduma zake kwa wateja lakini
pia kuhakikisha usalama katika huduma za kifedha kupitia maduka haya.
Hii ni fursa pekee kwa kwa wenye maduka
kushirikiana na Airtel na kuongeza mitaji yao lakini pia tunaamini kupitia
maduka haya yataongeza ajira kwa vijana na kuboresha usalama wakazi na
pesa zao kwani sasa wakazi wa maeneo ya hapa yatatunza pesa zao kwenye simu na
kuzitoa kwa urahisi kupitia maduka haya.
Uzinduzi
wa maduka ya Morogoro umefatiwa na uzinduzi wa maduka 8 mkoani Shinyanga
wiki iliyopita na huku mpango wake mzima ni kuwa na maduka mengine kama hayo ya
2000 nchi nzima.
No comments:
Post a Comment