Wachezaji wa Airel
Rising Stars kutoka Sierra Leone wakiwasili kwenye Uwanja wa Kimataifa wa
Julius Nyerere kuhudhuria kliniki ya soka ya kimataifa ya Manchester United
itayoanza Jumatano, 23-27 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXx
Wachezaji sita na
kiongozi mmoja kutoka Sierra Leone waliwasili jijini Dar es Salaam jana asubuhi
tayari kushiriki kliniki ya soka ya kimataifa ya siku tano itakayofanyika
kwenye uwanja wa Azam Complex kuanzia kesho, Jumatano 23 Aprili, 2014.
Washiriki kutoka Madagascar walitajiwa kutua jijini jana usiku.
Kwa mujibu wa
kuwasili kwa wachezaji, wengi wao wanatarajia kufika leo mchana na baadaye
usiku kuhudhuria mafunzo hayo yanayoshirikisha zaidi ya wachezaji 72 kutoka
nchi za Kenya, Uganda, Malawi, Sierra Leone, Burkina Faso, Chad, Congo
Brazzaville, DRC, Niger, Madagascar, Gabon, Seychelles na mwenyeji – Tanzania.
Wachezaji hao
chipukizi, wasichana na wavulana, walijipatia tiketi ya kushiriki kliniki baada
ya kufanya vizuri katika mashindano ya Airtel Rising Stars kwenye nchi zao
pamoja na timu zilizotwaa uchampioni wa mashindano ya kimataifa yaliyofanyika
nchini Nigeria mwaka jana.
Kliniki hii
itaendeshwa na wakufunzi kutoka klabu maarufu duniani ya Manchester United
ikiwa na lengo la kutoa mafunzo ya kuwawezesha wachezaji na kuwajengea uwezo wa
kutandaza kabumbu ya kusisimua hasa katika idara ya ushambuliaji.
Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mheshimiwa Bernard Membe atakuwa mgeni rasmi
katika hafla ya uzinduzi inayotarajiwa kuhudhuriwa na wageni mbalimbali kutoka
wizara inayohusika na michezo, shirikisho la mpira wa miguu nchini, Airtel
Tanzania na wadau wengine wa soka.
Hii ni fursa nyingine
muhimu kwa wachezaji hao chipukizi chini ya umri wa miaka 17 kuonyesha vipaji
vyao na kujiendeleza kisoka.
Program ya Airtel
Rising Stars ni mpango wa maendeleo ya soka kwa vijana chini ya umri wa miaka
17 barani Afrika ukidhaminiwa na kampuni ya simu za kiganjaji ya Airtel na
kuungwa mkono na Manchester United. Lengo lake ni kusaidia kuibua vipaji vya
soka kutoka ngazi ya chini (grassroots) hadi Taifa.
No comments:
Post a Comment