Picha ya pamoja baada ya kutoa msaada. |
Dar
es Salaam
Kampuni
ya simu za mkononi ya Airtel kupitia umoja wa wanawake ujulikanao kama Airtel
Divas umetoa msaada wa vifaa vya hospitali kwaajili ya wagonjwa wanaosumbuliwa
na magonjwa ya saratani katika hospitali ya Ocean road jijini Dar es salaam
Msaada
huu unafatia harambee kwa ajili ya kuchangisha pesa iliyofanywa na Airtel Diva
mwezi uliopita kwaajili ya kupata fedha za kuwasaidia wagojwa wanaosumbuliwa na
magonjwa ya kansa katika hospitali ya Ocean Road.
Akiongea
wakati wa kutoa msaada huo mwenyekiti wa Airtel Divas Amitin Mbamba alisema”
Tunatambua na tunapokea kwa machungu matatizo yanatowapata wanawake na watoto
wanaougua saratani na katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani kwa mwaka
2014 tuliamua kuchangisha pesa kwaajili yakutuwezesha kununua vifaa vya
hospitali na kuwasaidia wanawake na watoto pamoja na wagonjwa wengine hospitalini
hapa. Na leo tunayofuraha kutoa stretcher 2 pamoja na wheelchair 2 zenye
thamani ya shilingi million 5 hospitalini hapa.”
Tunaamini
msaada huu utawawezesha wahudumu kupata nyenzo muhimu na kuweza kufanya kazi
yao ya kutoa huduma kwa wagojwa kwa ufanisi zaidi.
“Nia
yetu ni kuhakikisha tunaendelea kutoa muda wetu na rasilimali katika kushikiri
na kuchangia shughuli za huduma kwa jaimii ili kukubailiana na matatizo
yanayoikumba jamii inayotuzunguka hususani wanawake wenzetu” aliongeza Mbamba
Mmoja
ya wajumbe wa Airtel Divas Bi Deliphina Martin Msuya alisema” tunayofuraha kuwa
sehemu ya kutoa msaada kwani tunatambua umuhimu wa wanawake katika kusimamia
familia, inagusa sana kuona jinsi gani wanawake wenzetu wanavyougua au
kuuguza watoto wao hospitalini hapa hivyo tunatoa wito kwa wanawake wengine
huku nje mmoja mmoja au kwa makundi kuwasaidia wanawake wenzetu walio katika
changamoto hizi kwani ni jukumu letu kusaidia wahitaji.
Akiongea
mara ya kupokea msaada huo Muuguzi Mkuu wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road
(ORCI), Mary Haule alisema” Hospitali yetu inaupungufu wa vifaa mbalimbali
zinavyotuwezesha kuhudumia wagonjwa tunashukuru sana Airtel kwa msaada wao na
kwa kuwezesha kupata hivi vifaa kwani vitatusaidia katika kutoa huduma na
kuongeza ufanisi wa kazi zetu za kusaidia wagonjwa hapa hospitalini. Nachukua
nafasi hii kuwaomba makampuni mengine na vikundi mbalimbali kusaidia changamoto
zingine zilizopo hospitalini hapa.
Airtel
Divas ni mpango ulioanzishwa Airtel Afrika nzima wenye lengo la kuwahamashisha
na kuwawezesha wanawake wanaotoka katika makuzi , mila na tamaduni mbalimbali
kujiamini na kufanikiwa katika maisha , mpango huu ulizindulia Airtel Tanzania
March 2012.
No comments:
Post a Comment