Wananci wakishangili mara baada ya Mkuu wa wilaya ya Songea
Joseph Mkirikiti kukata utepe kuashiria ufunguzi wa mnara wa Airtel.
|
xxxxxxxxxxxxxxxxxx
Mkuu wa Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma Joseph Joseph Mkirikiti amezindua
mitambo ya mawasiliano (minara) katikaka kijiji cha Muhukulu na
kuwataka raia wa Tanzania wa vijiji vya Muhukulu, Lalia, Magwamila, Nakwale,
Nambendo, Mkenda, Makwaya, Miputa vyote vya Mkoani Ruvuma na wale
wote wanaoishi mipakakani mwa Msumbiji na Tanzania kuwa Walinzi kwa
mitambo ya Airtel inayowekwa kwa ajili ya mawasiliano isiharibiwe na
watu wasiopenda maendeleo.
Mkuu
wa wilaya ya Songea Joseph Joseph Mkirikiti ameyasema hayo mwishoni
mwa wiki wakati akizindua Minara hiyo ya ya mawasiliano ya Simu
iliojengwa katika kata ya Mhukuru Mpakani mwa Msumbiji na Tanzania.
Mkuu
wa wilaya ya Songea Joseph Joseph Mkirikiti alisema “juhudi zinazofanywa
na Serekari kwa kushirikiana na Makapuni ya Simu ikwemo kampuni
ya Airtel ni kumpa mwananchi fulsa ya kuwasiliana na watukatika
mambo ya kiuchumi,afya,na elimu na mawasiliano ya kijami”
Amesema
pia katika kutatua kero mbali mbali za wananchi, pamoja na mawasiliano
ndiyo maana baada ya ziara ya Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa
Tanzania wananchi walipotoa kero zao kwa Rais ufumbuzi umefanywa wakuiomba
Airtel kujenga Mnara ..
…”sasa
ni juu ya Wananchi kuutumia kwa lengo lililo wekwa ili kutowakatisha
tamaa wawekezaji aliongeza kwa kusema Mkirikiti! Meneja
wa kanda ya kusini wa Airtel kutoka mbeya Straton Afrikan Mushi amewataka
wananchi kutumia mtandao wa Airtel hasa huduma za kibenki ili
kuepukana na uporaji wa fedha wanaposafili, pia amewaomba kuwa walinzi
wa Minara ya Airtel ‘naomba mfahamu huu mtambo hapa ni kwaajili
yenu wote hivyo changamkieni huduma zetu nafuu Zaidi hasa ile ya
Airtel Money ambayo itaondoa na kupunguza changamoto nyingi za upatikanaji
wa huduma za kibenk katika vijiji na miji ya karibu na mkoa
wetu huu” aliongeza Straton
Wananchi
wa Mkoani Ruvuma wameishukuru serikali kwa kuweza kushirikiana
na Kampuni ya Airtel kupata mawasilino ya uhakika huku injinia
wa Airtel Saidi Hanga akiwaahidi wananchi kuto katika kwa mawasiliano
Mnara
wa Simu wa Kampuni ya Airtel umekuwa mkombozi pekee kwa wananchi wa
Mpakani mwa Msumbiji na Tanzania ambao walikuwa wakisafiri kwa muda
mrefu zaidi ya kilometa 40 kutafuta sehemu yenye kushika mawasiliano
kwa kupanda kwenye kilele cha mlima, pia wamesema mawasiliano
ya nchi jirani ya msumbiji ukiyapata yalikuwa yatoza fedha
pande
zote mbili bila kujali nani kapiga simu nani amepokea simu.
No comments:
Post a Comment