Mkurugenzi wa Airtel huduma kwa
wateja Bi Adriana Lyamba akiongea na wafanyakazi wote pamoja na
wanahabari (hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa wiki ya huduma kwa
wateja leo katika makao makuu ya Airtel, Airtel inaadhimisha wiki hii
kwa kuwashuru wateja wake wote, kuongeza motishaa kwa watoa huduma wake
wote nchini kuendelea kuhudumia wateja, pamoja na kuhamasisha kila mtoa
huduma nchini kufahamu umhimu wa mteja.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Dar es
salaam
KAMPUNI ya simu za mkononi Airtel
imejipanga kikamilifu kushehekea wiki ya huduma kwa wateja kwa kuzitambua
jitihada na michango ya watoa huduma wao na kutambua
umuhimu
wa wateja.
Airtel
leo imefanya uzinduzi wa wiki hiyo na kuungana na ulimwengu mzima
kusherehekea wiki hii ya huduma kwa wateja. Airtel inaisherehekewa wiki
hii kipekee kabisa kwa kuhakikisha inatembelea
wateja
wao na kuendelea kuwapatia huduma bora zenye viwango vya hali ya juu
huku wakiongozwa na kauli mbiu ya "Mimi ni Airtel niko hapa kukuhudumia"
A am Airtel here for you".
Kitengo
cha Airtel huduma kwa wateja kimedhamiria kuitumia wiki hii kujifunza
changamoto tofauti toka kwa wateja pamoja na kuwapatia wateja wao wa nje
na ndani huduma stahiki kwa staili ya kipekee kabisa.
Akiongea
wakati wa uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja katika makao makuu ya
Airtel nchini Mkurugenzi mkuu wa Airtel Bw, Sunil Colaso alisema “kwetu
sisi Airtel wiki ya huduma kwa wateja
tunaithamini
na kuisherehekea na wateja wetu tukiwekea mkazo katika mambo muhimu
tunayotakiwa kuwafanyia wateja wetu kila wakati na sio tu ndani ya wiki
hii”
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Huduma kwa wateja Bi, Adriana Lyamba alisema
tunaanza kuisherehekea wiki hii hadi tarehe 10 octoba mwezi huu, wiki
itaambatana na mambo mengi yatakayofanywa na wafanyakazi wote wa Airtel
kwa lengo la kumfaidisha mteja
Wakurugenzi wa vitengo mbalimbali na mameneja
wao wako katika baadhi ya maduka yetu pamoja na sehemu muhimu za
kuhudumia wateja kwaajili ya kukutana na wateja na kuwahudumua kwa
wiki nzima alisema Bi, Lyamba
Katika
duka letu kuu Moroco Dar es salaam wateja wiki hii watahudumiwa na mimi
mwenyewe na timu yangu ya huduma kwa wateja alisisitiza Bi Lyamba
“Lengo
ni kumuhudumia mteja kwa ukaribu zaidi pamoja na kuwashukuru sana kwa
kuwa wateja wetu kwa muda mrefu na wakati mwingine kuwa wavumilivu
kwetu”,
Kwa kuongezea kipindi hiki cha wiki ya huduma
kwa wateja, Airtel inatoa bidhaa bora kwa OFA zikiwemo simu zetu za
Tecno H5 android smartphone. Simu hizi zimeshushwa bei na zinatoka
zikiwa na OFA kabambe ya kifurushi cha intaneti maalum.
Airtel Tanzania ndani
ya wiki hii ya huduma kwa wateja pia imetangaza kuwepo kwa motisha kwa
watoa huduma wote wa Airtel kwa lengo la kuwahamasisha kuendelea kutoa
huduma bora.
No comments:
Post a Comment