Tangazo

March 12, 2013

MKURUGENZI MKUU WA WIPO FRANCIS GURRY AWASILI NCHINI TANZANIA




Mkurugenzi Mkuu wa World Interllectual Property Organization (WIPO) Francis Gurry (wa pili kulia) akipokelewa na mwenyeji wake Mkurugenzi wa Uhamasishaji Biashara na Masoko wa Wizara ya Viwanda na Biashara Odilo Majengo (kulia) kwa niaba ya Waziri Dkt. Abdallah Kigoda mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndeege wa Kimataifa wa Mwl. JK Nyerere jijini Dar. Wa Pili kushoto ni Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou. (Picha na Zainul Mzige wa Mo Blog)
Mkurugenzi Mkuu wa World Interllectual Property Organization (WIPO) Francis Gurry na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou wakielekea katika chumba maalum cha wageni maalum kwenye Uwanja huo.
Mkurugenzi Mkuu wa World Interllectual Property Organization (WIPO) Francis Gurry akibadilishana mawazo baadhi ya maafisa mbambali wa Wizara.
Mkurugenzi Mkuu wa World Interllectual Property Organization (WIPO) Francis Gurry akizungumza na mwenyeji wake Mkurugenzi wa Uhamasishaji Biashara na Masoko wa Wizara ya Viwanda na Biashara Odilo Majengo.
Mkurugenzi Mkuu wa World Interllectual Property Organization (WIPO) Francis Gurry katika tete a tete na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Dkt. Alberic Kacou.
Mkurugenzi Mkuu wa World Interllectual Property Organization (WIPO) Francis Gurry akipitia moja ya magazeti maarufu nchini Tanzania la The Citizen ambalo limeandika habari kuhusiana na mkutano aliokuja kuhudhuria. Kushoto ni Dkt. Alberic Kacou.
Mkurugenzi Mkuu wa World Interllectual Property Organization (WIPO) Francis Gurry akisaini daftari la wageni katika chumba maalum cha wageni maalum mara baada ya kuwasili nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa World Interllectual Property Organization (WIPO) Francis Gurry akiteta jambo na Mkurugeni Mkazi wa Umoja wa Mataifa Dkt. Alberic Kacou wakati akijiandaa kuondoka katika Uwanja wa ndege. Kushoto ni Mkurugenzi wa Uhamasishaji Biashara na Masoko wa Wizara ya Viwanda na Biashara Odilo Majengo.
Mkurugenzi Mkuu wa World Interllectual Property Organization (WIPO) Francis Gurry akiingia kwenye gari maalum kuelekea hotelini.
Mkurugenzi Mkuu wa World Interllectual Property Organization (WIPO) Francis Gurry akiwasili hotelini na kulakiwa na baadhi ya maofisa wa WIPO.
Mkurugenzi Mkuu wa World Interllectual Property Organization (WIPO) Francis Gurry akipewa maelekezo machache kuhusiana na taratibu za mkutano wa kujadili Changamoto za Maendeleo katika Bara la Afrika katika mkutano nchini Tanzania.
Mkurugenzi Mkuu wa World Interllectual Property Organization (WIPO) Francis Gurry awasili nchini Tanzania leo kuhudhuria mkutano utakao zungumzia pamoja na mambo mengine Changamoto za Maendeleo katika Bara la Afrika.
Katika Mkutano huo wa siku mbili unaotarajiwa kuanza kesho pia wadau watazungumzia nafasi ya WIPO katika Kuchochea Maendeleo barani Afrika.
Mkutano huo utakaohitimishwa kesho kutwa utamalizika kwa kwa kuwa na kipindi cha majadiliano na kutoa maoni, ambapo wadau watatoa mitazamo yao kuhusiana na ajenda zilizowasilishwa na kutafuta mwelekeo wa pamoja.
 

No comments: