Tangazo

October 10, 2014

Airtel yahitimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja

Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Airtel Tanzania, Adriana Lyamba (katikati), Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Airtel, Kassim Mtingwa (wa tatu kushoto) na Meneja Uendeshaji Huduma kwa Wateja, Amit Arora wakikata keki kama ishara ya kufunga Wiki ya Huduma kwa Wateja katika hafla iliyofanyika kwenye Kituo cha Huduma kwa Wateja cha Airtel kilichopo Quality Centre Barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Airtel Tanzania, Adriana Lyamba (kushoto), akitoa huduma kwa wateja wa kampuni hiyo wakati wa kufunga Wiki ya Huduma kwa Wateja, katika hafla iliyofanyika kwenye Kituo cha Huduma kwa Wateja cha Airtel kilichopo Barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Airtel Tanzania, Adriana Lyamba (kushoto), akimkabithi kifurushi cha zawadi mteja wake Bwana Aliasger Hussein ambaye ni Meneja mwendeshaji wa kampuni ya Royal Procurement Ltdwakati Airtel ilipotembelea wateja wake katika wiki ya huduma kwa wateja.
Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Airtel Tanzania, Adriana Lyamba pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa kitengo cha huduma kwa wateja  na maongezi na  Bwana Aliasger Hussein wakati Airtel ilipomtembelea ofisini kwake katika wiki ya huduma kwa wateja. Pichani ni Meneja huduma kwa wateja Jacob Sumary  na  Afisa huduma kwa wateja bi Neifita Olomi

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Dar es Salaam


Katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imehitimisha wiki hii inayosherehekewa duniani kwa kuwatembelea wateja wake mbali mbali na kuwashukuru kwa kutumia huduma na bidhaa zake.

Airtel imetembelea wateja wake katika maeneo mbalimbali ikiwa pamoja na Tandika, magomeni, Temeke ,Sinza, Mbagala, illala , kinondoni na katika maeneo yenye watu wengi na kuongea nao kwa nyakati tofauti lengo likiwa ni kupata maoni juu ya huduma na pia kuwaelimisha kuhusu huduma na ofa mbalimbali.


 Alikadhalika wakurugenzi wa Airtel walitembelea wateja katika ofisi zao na kutembelea call center kituo cha kuhudumia wateja waaopiga simu na kuongea  na wateja wanaopiga namba 100 kwa msaada zaidi.

Akizungumza wakati wa kuhitimisha wiki hii Mkurugenzi wa kitengo cha huduma kwa wateja Bi Adriana Lyiamba alisema” tumekuwa na wiki ya mafanikio makubwa kwani tumepata nafasi nzuri ya kuendelea kuonana na kuongea na wateja wetu ana kwa ana na kuwazawadia ikiwa ni kuwashukuru kwa kuwa pamoja nasi na kutumia huduma zetu.


Tunaahaidi kuendelea kutoa huduma bora zilizo za kisasa na za kibunifu huku tukitoa huduma kwa wateja zenye uzoefu tofauti kupitia kituo chetu cha kupokea simu (call center) maduka yetu na sehemu zote ambazo wateja wanapata huduma zetu. Tunapomaliza wiki hii maalumu kwa huduma kwa wateja tunapenda kuwahakikishia watanzania huduma bora kwani tunatambua huduma bora ni mwendelezo wa maisha ya kila siku na si kwa wiki hii tu.

Akiongea wakati alipotembelewa ofisini kwake Bwana Aliasger Hussein Gomberawala alisema” tunafurahi kwa uongozi wa Airtel kuwa nasi leo hapa, tumekuwa wateja wa Airtel kwa muda na tunafurahishwa na huduma zao kwa ujumla, matatizo ya kimtandao katika technologia hii yapo  mengine ni ya uelewa wa vifaa vya kisasa na technologia hivyo elimu inatakiwa kutolewa ili wateja waende sambamba na mabadiliko haya.


Tunaomba Airtel waendelee kutuletea huduma za kibunifu na kuendelea kupunguza gharama za mawasiliano kwani tunategemea sana haya mawasiliano katika kuendesha biashara zetu. 

No comments: