Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi, Abdallah Mwinyi akijiandaa
kukata utepe kuashiria uzinduzi wa duka la huduma kwa Wateja la Airtel kisiwani
Zanzibar(Kushoto) Mkurugenzi wa huduma kwa wateja wa airtel Tanzania, Adriana Lyamba
(kulia) Maneja wa Kanda ya Zanzibar Mariam Yussuf.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
•Wateja kufurahia ubora wa juu wa huduma kutoka
Airtel kisiwani Zanzibar.
Airtel Tanzania imefungua duka lake la
kisasa kisiwani Zanzibar lililopo mtaa wa Mlandege lenye uwezo wa
kuhudumia wateja zaidi ya 100 kwa siku.
Ni duka la kisasa ambalo lipo karibu na
wateja lenye kurahisisha maisha ya wateja wote wa Airtel kisiwani Zanzibar.
Akizungumza katika uzinduzi wa duka hilo
Mkurugenzi kwa huduma kwa wateja , Bi Adriana Lyamba alisema, "kwamba
kupanua kwetu kwa huduma za mtandao kwa wateja wetu ni ishara tosha
ya kuonyesha ni jinsi gani Airtel inajali wateja wake na kuwapatia wateja wetu
huduma bora na za
kibunifu.
"Ni juhudi zetu na mafanikio
yetu ya kuwa na wateja zaidi ya milioni 9 tulionao ndio yanayotufanya tuweze
kuwashukuru wateja wetu kwa kuwapatia huduma nzuri zenye Kiwango cha juu. Kwa
huduma unazozitoa kupitia maduka yetu yaliyoenea hapa nchini maduka haya
yanauwezo wa kutoa huduma zenye kiwango cha juu
yanayotoa huduma kwa masaa mengi na kutoa huduma nzuri kwa wateja. Uzinduzi wa
maduka yetu ni mafanikio makubwa kwetu na hii ni shukurani yetu kwao kwa
kuwaonyesha ni jinsi gani tunawajali wateja wetu.
Hafla hiyo ilizinduliwa na Mkuu wa Mkoa
Mjini Magharibi Abdallah Mwinyi, ambaye aliipongeza Airtel kwa ajili ya kuleta
huduma zake karibu na watu wa Zanzibar.
"Mbali na kutatua matatizo ya wateja,
mtazamo huu mpya wa duka hili ni maendeleo tosha kwa wakazi wa Zanzibar kwani
huduma zinazotolewa hapa ni za kiwango kizuri na uwezo mkubwa ambapo wateja wa
Airtel wamekuwa wakihitaji hapa kisiwani Zanzibar. alisema.
Mwinyi alisema kuwa, huduma mbalimbali za
mawasiliano zinazotolewa na Airtel kuanzia , ujumbe, Inteneti , usajili, huduma
za Airtel Money ambazo zinarahisisha maisha ya wananchi katika jamii.
"Huduma hizi zinaleta
matokeo mazuri katika namna ya kufanya biashara na kuboresha maisha ya maelfu
ya wakazi wa Zanzibar na mamilioni ya Watanzania kwa ujumla," aliongeza
Mwinyi.
Kama sehemu ya huduma nzuri , Airtel tayari
imekarabati maduka mengine katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Bukoba,
Mbeya, Mtwara, Dodoma, Mwanza, Tabora na leo hapa Zanzibar.
Maduka ya Airtel yataendelea kutoa huduma
mbali mbali zenye kiwango cha juu na upatikanaji wa bidhaa zake kama vile
modems, simu, malipo ya bili,huduma za Airtel money na huduma nyingine nyingi .
Tumewekeza kwa kiwango kikubwa katika
mtandao wetu ili kuhakikisha wateja wetu wanapata huduma sahihi na ya kiwango
cha juu.
No comments:
Post a Comment