Tangazo

October 7, 2014

BENKI YA CRDB YAADHIMISHA SIKU YA WATEJA

Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB anayeshughulika na Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, Saugata Bandyadhiyay (kulia) akizungumza na  wateja waliofika katika tawi la Holland House jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wateja wa Benki ya CRDB. 
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB ,Esther Kitoka (kushoto) akitoa ufafanuzi kwa wateja waliofika katika tawi la Tabata jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wateja wa Benki ya CRDB ambapo viongozi wa benki hiyo wamekuwa wakitoa huduma za kibenki katika matawi mbalimbali ya benki hiyo. 
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB anayeshughulika na Uendeshaji na Huduma kwa WatejaSaugata Bandyadhiyay (wa pili kulia) akisalimiana na wateja waliofika katika tawi la PPF Tower jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wateja wa Benki ya CRDB. Kulia ni Mkurugenzi wa tawi la PPF Tower, Can Meseyeck. 
 Meneja wa Benki ya CRDB tawi Tabata, Hawa Sasya akisalimiana na watoto wa shule ya African Nursery & Primary School ya Tabata jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Wateja wa Benki ya CRDB iliyoanza Oktoba 6.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB anayeshughulika na Uendeshaji na Huduma kwa WatejaSaugata Bandyadhiyay (kushoto), Mkurugenzi wa tawi la Holland House, wakiwa katika picha ya pamoja na maofisa wa Benki ya CRDB.
Mkurugenzi wa kituo cha Radio cha Sport FM cha Dodoma, Abdallah Majura (kulia) akipongezwa na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB anayeshughulika na Uendeshaji na Huduma kwa WatejaSaugata Bandyadhiyay wakati maadhimisho ya Siku ya Wateja wa Benki ya CRDB wakati Mkurugenzi huyo alipotembelea tawi la Azikiwe Premier jijini Dar es Salaam.



Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB anayeshughulika na Uendeshaji na Huduma kwa WatejaSaugata Bandyadhiyay (kushoto) akikata keki na Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Azikiwe Premier, Fabiola Mussula wakati maadhimisho ya Siku ya Wateja wa Benki ya CRDB.
Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Azikiwe Premier, Fabiola Mussula akimlisha keki Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyoSaugata Bandyadhiyay ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wateja wa Benki ya CRDB.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyoSaugata Bandyadhiyay akimlisha keki  Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Azikiwe Premier, Fabiola Mussula.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDBSaugata Bandyadhiyay (wa nne kutoka kulia), Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Azikiwe Premier, Fabiola Mussula (wa tatu kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na wateja wa benki hiyo pamoja na maofisa wa CRDB.

Maofisa wa Benki ya CRDB wakiwa wamepozi kwa picha.
Picha ya pamoja
Wateja wa Benki ya CRDB wakipata huduma katika tawi la Holland House.
Mkurugenzi Mkuu wa Msae Investment, Wilbard Mtenga akipokea keki kutoka kwa  Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDBSaugata Bandyadhiyaywakati wa maadhimisho ya Siku ya Wateja wa benki ya CRDB.

Na Mwandishi Wetu

BENKI ya CRDB inaadhimisha wiki ya huduma kwa wateja kwa kusikiliza matatizo yanayowakabili wateja wa benki hiyo.

Akizungumza alipotembelea matawi ya Holland, Premier na PPF Tower jijini Dar es Salaam, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Saugata Bandyadhiyay, alisema kuwa wanatumia wiki hiyo katika kusikiliza matatizo ya wateja ili kuboresha huduma.

Bandyadhiyay alisema pia watasikiliza kero za wateja pamoja na kupata maoni juu ya huduma inayotolewa na benki hiyo ikiwa ni pamoja na kuyatatua.

Alisema CRDB itahakikisha inatoa huduma kwa usikivu, uwajibikaji, nia, ubunifu ushirikiano na ufanisi ili kuongeza tija kwa wateja wanaowahudumia.

Naye Meneja wa akaunti tawi la Premier, Nellie Mwambapa, aliwataka wateja kuhakikisha wanafika na kuandika maoni yao ikiwa ni pamoja na kuleza mapungufu ili CRDB iendelee kutoa huduma bora.

1 comment:

Meizitang Botanical said...

i like it this blog and article