Tangazo

October 17, 2014

MKURUGENZI MKAZI WA UNESCO AMTEMBELEA MKUU WA MKOA WA DODOMA

DSC_0206
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues (katikati) akiongoza na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mtungi (kulia) baada ya kuwasili ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Rehema Nchimbi. Kushoto ni Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) Bw. Al Amin Yusuph.
DSC_0209
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Rehema Nchimbi akimkaribisha ofisini kwake Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO Tanzania, Zulmira Rodrigues alipomtembelea na kufanya naye mazungumzo. Kushoto ni Msajili wa Vyama vya Siasa nchini. Jaji Francis Mtungi na kushoto ni Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) Bw. Al Amin Yusuph na Nyuma kabisa ni Msajili Msaidizi kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Sisty Leonard Nyahoza.
DSC_0232
Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO Tanzania, Zulmira Rodrigues akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Rehema Nchimbi alipomtembelea leo na kufanya nae mazungumzo juu masuala mbalimbali ya maendeleo likiwemo suala la elimu na changamoto zake katika mkoa wa Dodoma.
DSC_0237
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mtungi (wa pili kulia) akibadilishana mawazo na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Rehema Nchimbi (kushoto), Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO Tanzania, Zulmira Rodrigues (wa pili kushoto) pamoja na Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) Bw. Al Amin Yusuph, Msajili Msaidizi kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Sisty Leonard Nyahoza walipomtembelea Mkuu huyo wa mkoa ofisini kwake leo.
DSC_0248
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues (wa pili kushoto) akitoa maelezo ya kazi mbalimbali zinazofanywa na shirika lake ikiwemo Mradi wa Micro Science Kits (MSKs) ulioendeshwa kwa miaka minne wa kusaidia ufundishaji wa masomo ya sayansi kwa kufanikisha majaribio ya maabara uliokuwa ukifadhiliwa na Shirika lake na kuendeshwa na Wizara ya Elimu nchini katika shule 180 zilizopo katika wilaya 34 ambao umemalizika hivi karibuni kwa mafanikio makubwa.
DSC_0280
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Rehema Nchimbi katika picha ya pamoja na ugeni huo ofisini kwake mjini Dodoma leo.
DSC_0330
Mkurugenzi Mkazi wa UNESCO Tanzania, Zulmira Rodrigues akisisitiza jambo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Rehema Nchimbi alipokuwa akigana nae mara baada ya mazungumzo ofisini kwake mjini Dodoma.

No comments: