XXXXXXXXXXXXXXXXXX
Dar es Salaam
Desemba 2014
Kampuni
ya simu za mkononi ya Airtel imetoa vifaa vya michezo kwa chuo kikuu
cha Dar es Salaam ili kuendesha mashindano yatakayoshirikisha vitivo
mbalimbali yanayotegemea kuanza jumatatu ijayo katika viwanja vya Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam
Mchango
huu ni mwendelezo wa dhamira ya Airtel katika kuendeleza michezo nchini
inayodhirishwa kupitia mpango wake wa kuinua soka la vijana chini ya
miaka 17 wa Airtel Rising Stars mpango ambao umewawezesha vijana
wakitanzani na Afrika kwa ujumla kuonyesha uwezo wao wa kisoka na kuweza
kufikia malengo yao.
Akiongoe
wakati wa makabidhiano hayo Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando
alisema” Leo tunatoa vifaa vya michezo ikiwemo seti 12 za jezi,
shinguard, soksi, glovu za goalikipa pamoja na makombe yatakayowezesha
kuendesha mashindano haya yanayoshirikisha wanafunzi kutoka vituvo
mbalimbali chuoni hapa. Niwazi kwamba michezo ni burdani na ni sehemu ya
kujenga mwili na afya hivyo ni muhimu pia kwa wanafunzi kutenga muda
wao wa masomo na kushirikia katika michezo mbalimbali. Natoa wito kwa
wanafunzi wengi kujitokeza na kushiriki mashindano haya.”.
“Udhamini
wetu leo ni mwanzo wa mkakati wa kutoa ofa kabambe itakayowapatia
wanavyuo uhuru wa kuongea na kupata dhamani yamatumizi ya pesa zao
Ofa
hii ya huduma maalumu ijulikanayo kama UN255 Itazinduliwa rasmi wakati
wa kilele cha michuano hiii mwishoni mwa wiki ambapo wanafunzi
watafurahi huduma zetu nyingi ikiwa ni pamoja na internet, ujumbe mfupi ,
kupiga simu kwa gharama nafuu. Aliongeza Mmbando
Kwa
upande wake Naibu Makamu mkuu wa chuo Profesa Yunus Mgaya alisema”
nawashukuru sana Airtel kwa mchango wa mkubwa na kwa kutuwezesha kupata
vifaa vya michezo zitavyotuwezesha kuvitumia muda wote wa mashindano.
Sisi kama chuo hatukuwa na bajeti ya kununua vifaa hivi hivyo msaada huu
umekuja kwa wakati muafaka hivyo nawapongeza sana Airtel kwa mchango
wao.”
“Vifaa
hivi vitaleta tija kwa wanafunzi na kuinuua michezo chuoni hapa na ofa
hii UN255 itawawezesha wanafunzi na pamoja na familia yetu yote ya
chuo kikuu cha Dar es saalam kufurahia huduma za mawasiliano bora na kwa
bei nafuu” aliongeza Mgaya
No comments:
Post a Comment