Meneja
Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando (kulia) na Meneja Masoko wa Airtel, Aneth
Muga (kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Airtel Trace
Music Stars mara baada ya washiriki hao kuongea na waandishi wa habari kwaajili
ya kuomba wananchi kuwapigia kura.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Dar es Salaam
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel mapema wiki
hii, imetangaza washiriki walioingia kumi bora wiki hii katika mashindano ya
Airtel Trace Music Stars yenye lengo la kuvumbua na kusaka vipaji vya
wanamuziki chipukizi nchini na Afrika kwa ujumla.
Shindano hilo lililozinduliwa mwanzoni mwa mwenzi
wa Kumi, linaendelea kuwapatia watanzania na wapenzi wa muziki nafasi ya
kushiriki kwa kupiga namba 0901002233 na
kurekodi wimbo na kuutuma kisha wimbo huo kutasminiwa na jopo la majaji
na kufudhu kuingia katika hatua ya kupigiwa kura.
Akiongea na waandishi wa habari Meneja Masoko wa
Airtel Bi Anneth Muga alisema” tunafurahi kuona jinsi gani watanzania
wanavyoitikia na kushiriki katika shindano hilo ambapo mpaka sasa limedumu kwa
takribani mienzi miwili na nusu. Leo hii tunao wanamuziki chipukizi ambao wameweza
kuibuka kuwa katika kumi bora ya wiki hii na tunapenda kuwatangazia jamii,
wapenzi wa muziki ili muweze kuwapigia kura na waweze kuendelea kufanya vizuri
katika mashindano haya.
Napenda kuchukua fulsa hii kuwakumbusha
watanzania kwa Mshindi wa Airtel Trace Music Stars atapatikana kwa vigezo
viwili vikubwa kwanza ni kwa uwezo wake wa kuimba na pili kutokana
na wingi wa kura , hivyo tumeona ni vyema sasa kuwaleta kwenu ili muweze
kuwawezesha kutimiza ndoto zao waendelee kwa kuwapigia kura ilie kufanya
vizuri kwenye mashindano haya.
Kwa upande wake Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson
Mmbando alisema “ kwa sasa tuko kwenye hatua muhimu sana ya kuwawezesha
washiriki hawa kuendelea mbele kwa kupiga kura, kura yako ndio inahitajika sasa
ni rahisi sana unaweza kupiga kura kwa kupiga namba 0901002233 Kisha ukachagua lugha na kufata maelekezo,
ili kuupigia kura wimbo au mshiriki ni lazima uwe na kodi ya namba yake ya
ushiriki hakikisha una kodi namba ya mshiriki unayetaka kuumpia kura wakati
wote wa kupiga kura kisha utapata maelekezo ya kuingiza kodi hiyo na baada ya
kuingiaza utasikia wimbo wa mwimbaji na kuamua kumpigia kura. Njia ya pili ni
kwakuandika ujumbe wenye kodi namba ya ushiriki na kisha kuituma kwenye namba 15594
na tayari utakuwa umepiga kura yako.
Tutaendelea kuwajulisha washiriki watakao ingia
kumi bora kila wiki na ili kupata habari hizi kwa urahisi basi tembelea
facebook page yetu ya Airtel Tanzania na upata kuona picha za washiriki
mbalimbali, namba zao za ushiriki na kusikiliza nyimbo zao kupitia simu yako ya
mkononi. Natoa wito kwa watanzania kuendelea kushiriki kwenye mashindano haya
kwa kujisajili na kurekodi na kwa kupigia kura washiriki ili tupate mwakilishi
bora atakayekwenda kutuwakilisha kwenye mashindano ya Airtel Music Trace Afrika
yatakayoshirikisha nchi 17 za Afrika hapo mwaka kesho “ aliongeza mmbando.
Akiongea wakati wa maojiano na waandishi wa
habari mmoja kati ya washiriki kumi bora wa wiki hii Jesca Charles alisema”
najisikia furaha sana kuingia katika kumi bora ya wiki hii, naomba watanzania
wanipigia kura kwa wingi ili nisishuke nieendelee kufanya vizuri. Napenda sana
kuimba na ndoto yangu ni kuwa mwimbaji wa kimataifa na mwimbaji nae vutiwa nae
ni Beyonce natumaini siku moja ntafikia na kuwa mwimbaji nyota kama Beyonce”
Washiriki Walioingia kumi bora wiki hii ni pamoja
na Christopher kihwele namba ya ushiriki 55100050, karen Gardner 55100107,
Mwinyimkuu Hussein 55100048, John chambasi 55100005, Vanessa Galinoma 55100232,
Jesca Charles 55100135, Anne Mkisi 55100004.
Mashindano ya Airtel Trace yatafikia kilele
mwanzo mwa mwaka kesho ambapo mshindi wa Airtel Trace Afrika atajishindia
zawadi kabambe ikiwemo, kurekodi na kusambaziwa nyimbo zake chini ya studio
kubwa ulimwenguni pamoja na safari kwenda nchini marekani na kupata mafunzo
ya kimuziki na Nguli wa Muziki wa Amerika Akon.
No comments:
Post a Comment