Mratibu wa Uhuru marathon Tanzania Innocent Melleck
akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam juu ya kukamilika kwa
maandalizi yam bio hizo zinazotarajiwa kufanyika jumapili hii jijini Dar Es
Salaam katika viwanja vya Leaders Club. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la
Riadha la Taifa (AT), Selemani Nyambui.
xxxxxxxxxxxxxxxx
Na Mwandishi Wetu
MAANDALIZI ya mbio za
Uhuru, Uhuru Marathon, zinazotarajiwa kufanyika kesho jijini Dar es Salaam
yamekamilika, huku wanaridha kadhaa kutoka ndani na nje ya nchi wakithibitisha
kushiriki mbio hizo zenye lengo la kuulinda uhuru wetu, kudumisha umoja, amani,
upendo na mshikamano miongoni mwa Watanzania.
Akizungumza na waandishi
wa habari jana, Mratibu wa Uhuru Marathon, Innocent Melleck alisema, maandalizi
yote yamekamilika, huku wanariadha wa hapa nchini kutoka nje ya Dar es Salaam
wakiwa wamewasili tayari kwa ushiriki wao.
Melleck pia alisema, kwa
kushirikiana na Jeshi la Polisi ulinzi umeimarishwa kwa kiwango kikubwa ili
kuhakikisha usalama unakuwa mkubwa kwa washiriki wote na barabara
zitakazotumika zitafungwa katika kipindi hicho.
“Kila kitu kimekamilika na
washiriki kutoka nje ya Dar es Salaam wameanza kuwasili kwa ajili ya mbio hizo
na tunawahakikishia usalama utakuwa mkubwa mno katika kipindi chote cha mbio
hizo n mpaka kufikia jana (juzi) tayari washiriki waliojitokeza walikuwa 4000,”
alisema.
Katibu Mkuu wa Chama cha
Riadha Tanzania (RT), Selemani Nyambui alisema, wanariadha maarufu wa hapa
nchini watakaoshiriki ni pamoja na Fabian Joseph na Dickson Marwa, huku Jacqueline
Sekini aliyeshinda mbio hizo kwa upande wa wanawake mwaka jana, naye akiapa
kutetea ubingwa wake.
“Wapo wanariadha wengi
watakaoshiriki, lakini nataka kutoa angalizo kwa wanariadha kutoka Kenya, sisi
tumetumwa mwaliko kwa wa chama husika na wao ndio watutumia majina ya
wanariadha kumi, watano wa kiume na waliobaki wa kike, hatutapokea mwanariadha
kutoka nchi hiyo ambaye hatujapewa jina lake,” alisema.
Nyambui alisema, tayari
waamuzi atakaosimamia mbio hizo wapo tayari na akasisitiza ni lazima
taratatibu zote zitafuatwa ili kupata mshindi halali.
Mbio hizo zinatarajiwa
kuanzia viwanja vya Leaders Club na zitakuwa za kilomita 21, kilomita 5 na
kilomita 3 ambazo ni maalumu kwa ajili ya viongozi wa kitaifa, dini na taasisi
mbalimbali.
Aidha Melleck alisema,
tayari namba kwa washiriki zimeanza kutolewa na wanaweza kuzipata katika
viwanja vya Leaders Club. Mgeni rasmi katika mbio
hizo anatarajiwa kuwa Rais Jakaya Kikwete.
No comments:
Post a Comment