· Wateja kutuma pesa bila kikomo kwenda Airtel bure bila makato yoyote.
Kampuni
ya simu za mkononi ya Airtel kwa mara nyingi tena imewazawadia wateja
wake wakatia wa msimu huu wa sikukuu na OFA maalum itakayowawezesha
kutuma pesa bila kikomo BURE kupitia Huduma ya Airtel Money.
Akiongea
wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo Mkurugenzi wa Mawasiliano Bi
Beatrice Singano Mallya alisema” Tumeona ni vyema kuwazawadia wateja
wetu nchin nzima na kuwawezesha kutuma pesa BURE wakati wa msimu huu wa
sikukuu kwani tunatambua wateja wetu na watanzania wanafanya miamala ya
pesa kwa wingi wakati wa kipindi hiki cha msimu wa Sikukuu za Xmass na
Mwaka mpya na kusherehekea nao. kuanzia sasa wateja wetu wataweza kutuma
pesa kwa ndugu jamaa na familia popote nchini Airtel –Airtel BURE
kabisa.
Hii
ni nafasi pekee kwa wateja wetu na tunaamini kabisa kwamba ofa hii
itawapatia wateja wetu thamani ya pesa zao na kuwawezesha kupata pesa ya
akiba kwa matumizi mengine katika msimu huu wa sikukuu”
Pamoja
na ofa hii pia ya Airtel Money pia tumeweza pia kuwazawadia wateja wetu
Katika msimu huu wa sikukuu na Ofa kabambe ya simu za kisasa kwaajili
ya wapendwa wao zinazopatikana katika maduka yetu zikiambatana na
vifurushi , Ofa kabambe nchini . na uzinduzi wa Ofa hii ya Airtel Money
leo ni mwendelezo wa shamrashamra za kusherehekia msimu wa sikukuu na
wateja wetu.
“Sambamba
na hilo huduma yetu ya Airtel Timiza bado inaendelea, wateja wanaweza
kukopa pesa na kukidhi mahitaji .Mikopo hii ni salama, haina akiba na
ina riba nafuu na inapatikana katika kiganja chako cha mkono kupitia
simu yako ya mkononi. Hivyo tumewawezesha wateja wetu si kutuma pesa
bure tu bali kupata pesa wakati wowote wanapohitaji.
ili
kufurahia ofa hii ya Airtel Money mteja anatakiwa kupiga *150*60# na
moja kwa moja utakuwa umeunganishwa na orodha ya huduma za Airtel Money
na utume pesa sehemu yoyote BURE”. Ofa hii itadumu kwa muda wa mwenzi
mmoja.
No comments:
Post a Comment