· Chini ya mpango wake
wa shule yetu, shule za sekondari manyara, Moshi na Tanga kupokea msaada huo
mwenzi huu
Wanafunzi na walimu
wa shule ya Sekondari Nanja wamepokea msaada wa vitabu kutoka Airtel, Msaada
utakaoweza kuchangia katika kutatua tatizo la uhaba wa vitabu shule ni hapo.
Akitoa taarifa ya
shule , Mkuu wa shule ya sekondari ya Nanja Bwana Yona luka alisema” shule yetu
ina jumla ya wanafunzi 549 na walimu 32, matokeo ya shule ya kidato cha
nne yanakuwa kila mwaka ufaulu wa asilimia 71% pamoja na kukua kwa kiwango cha
ufaulu bado shule inachangamoto nyingi ikiwemo uhaba wa vitabu na walimu.
Kwa sasa uwiano wa vitabu vya sayansi ni kitabu 1 kwa wanafunzi 5 wakati
kwa vitabu vya sayansi ya jamii uwiano ni kitabu 1 wanafunzi 30. Tunafurahi sana
kupokea vitabu hivi toka Airtel kwani msaada huu umekuja kwa wakati muafaka”
Akiongea wakati halfa hiyo fupi ya
kukabithi vitabu , Afisa Elimu wa shule za sekondari halmashauri ya Monduli
Bwana Shaban Kasim Mgunya alisema” napenda kuwashukuru sana Airtel kwa
kufikisha msaada huu wa vitabu kwa sekondari hii ya Naja , vitabu hivi vya
sayansi havitachangia kuongeza kiwango cha ufaulu tu bali vitawahamasisha
wanafunzi wengi kujiunga na masomo ya sayansi.
Natoa wito kwa walimu kuwapatia
wanafunzi vitabu hivi wavisoma ili kuwajengea wanafunzi hawa tabia ya kusoma
vitabu. Nawahasa wanafunzi kuvitunza vitabu ili viweze kutumika na wanafunzi
wengi zaidi shuleni hapa.
Aliongeza kwa kusema” shule imeweza
kujenga maktaba lakini tunayochangamoto ya uhaba wa vifaa vya maktaba ,
nachukua fulsa hii kuwaomba Airtel waendelee kutusaidia kwa kuchangia vifaa vya
mahabara na kuwezesha masomo ya sayansi ya vitendo”
Akiongea kwa niaba ya Airtel Meneja wa
kanda ya kaskazini Brighton Majwala alisema”wote tunatambua tatizo la uhaba wa
vitabu katika shule za sekondari ambapo hali halisi haiendani namahitaji,
uwiano wa kitabu 1 ni kwa wanafunzi 10. Kwa kuliona hilo Airtel tumejikita na
kushirikiana na serikali katika kuhakikisha tunatutua changamoto hii na
kuongeza kiwango cha ubora wa elimu nchini. Natoa wito kwa wanafunzi wa
Nyala kuzitumia vitabu hivi vizuri na kuboresha kiwango cha ufaulu.
Kwa upande wa wanafunzi wameishukuru
Airtel kwa kuboresha elimu na kusema vitabu hivi vitawasaidia kuongeza ujuzi
katika masomo ya sayansi na kufanya vizuri zaidi.
Halfa ya kukabithi vitabu katika shule ya
sekondari Nanja ilimalizika kwa zoezi la kupanda miti ambapo walimu, wanafunzi
na Airtel walishiriki katika kuboresha mazingira ya shule.
Airtel chini ya mpango wake wa Airtel
Shule yetu mpaka sasa imezifikia shule zaidi ya 1300 nchini, shule nyingine
katika kanda ya kaskazini zitakazofaidika na vitabu hivi ni pamoja na
Manyara, Moshi na Tanga na shule nyingine katika maeneo mbalimbali ya nchi nazo
zitaendelea kupata msaada huu wa vitabu.
No comments:
Post a Comment