Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akihutubia wananchi katika Kijiji cha Changarikwa wakati wa ziara ya kikazi pamoja na kuwashukuru wananchi kwa kuchagua viongozi wa Seikali ya Kijiji wa CCM katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.CCM imepata ushindi wa Vijiji vyote katika 74 katika jimbo hilo.
Ridhiwani akisisitiza jambo alipokuwa akihutubia katika kijiji hicho ambapo aliwataka kuacha tabia ya kukata miti ovyo kwa ajili ya mkaa ama sivyo vijiji vitageuka jangwa.
Mkazi wa Kijiji cha Kwaluhongo, Dustan Sangi akiuliza swali kwa Mbunge wake Ridhiwani Kikwete wakati wa mkutano uliofanyika kijijini hapo
Ridhiwani akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kwaluhonbo ambapo alijibu maswali mbalimbali ya wananchi kuhusiana na kero mbaalimbali walizonazo pamoja na suluhisho
Ridhiwani akizungumza jambo na Khamis Ibrahim baada ya mkutano kumalizika katika Kijiji cha Kwaluhongo, wakati wa ziara yake ya kikazi katika Kata ya Mbwewe, Chalinzi, wilayani Bagamoyo jana.
Mama mkazi wa Kijiji cha Changarikwa akiuliza swali kwa mbunge kuhusu tatizo la kijiji hicho kutokuwa na Zahanati
Katibu wa CCM Wilaya ya Bagamoyo,Kombo Kamote akiwafunda viongozi wapya wa Serikali ya Kijiji cha Changarikwa ambapo aliwataka kujali sana maendeleo ya wananchi badala ya maslahi yao binafsi.
Wazee wakisikiliza kwa makini wakati Ridhiwani akihutubia katika Kijiji cha Changarikwa, Kata ya Mbwewe.
Ridhiwani akiifariji familia ya marehemu Jangili Shaban alipokwenda kuhani msiba baada ya kumalizika kwa mkutano katika Kijiji cha Changarikwa
Mzee Athuman Mnemwa akielezea mbele ya Mbunge wake Ridhiwani Kikwete jinsi Kijiji cha Kwang'andu kinavyoteseka na kero ya maji.
Mwanahawa Habib akielezea mbele ya Ridhiwani jinsi wakazi wa kijiji hicho wanavyonyapaliwa na Daktari na wauguzi wa Zahanati ya kijiji hicho
Mzee Athuman Kisuli akisisitiza umuhimu wa kupelekewa maji katika Kijiji cha Kwang'andu
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Pwani, Subira Mgalu akiwasalimia wananchi wakati wa mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kwang'andu ambapo aliahidi kusaidiana na Ridhiwani kutatua tatizo la maji linalowakabili wananachi wa kijiji hicho
Ridhiwani akihutubia katika mkutano huo na kuahidi kutatua kero mbalimbali ikiwemo ya maji katika kijiji hicho cha Kwang'andu, Kata ya Mbwewe
Mwananmke aliyejitangaza kuwa anaishi na virusi vya Ukimwi Pili Mbwana akiomba mbunge Ridhiwani kusaidia kuwasaidia kupata mikopo watu wanaoishi na VVU katika Kijiji cha Kunduchi Kata ya Mbwewe ili iwasaidie kuondokana na umasikini walio nao
Ridhiwani akihutubia wananchi katika Kijiji kipya cha Kunduchi wakati wa ziara yake atika Kata ya Mbwewe jana
Wananchi wakimsikiliza kwa makini mbunge wao
Ridhiwani akizungumza na Pili Mbwana anayeishi na virusi vya Ukimwi ambapo aliahidi kumsaidia jinsi ya kupata mkopo
Ridhiwani akiteta jambo na Mzee Suleiman Kadagala baada ya kumalizika kwa mutano huo.
No comments:
Post a Comment