Dk. Winnie Mpanju-Shumbusho
kutoka Tanzania ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu Msaidizi wa Shirika la Afya
Duniani (WHO), Geneva, Uswisi
XXXXXXXXXXXXXXXXXXX
Na
Mwandishi Wetu
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Afya Duniani, Dk. Margaret F. Chan amemteua Dk. Winnie Mpanju-Shumbusho
kutoka Tanzania
kuwa Mkurugenzi Mkuu Msaidizi wa Shirika la Afya Duniani, upande wa masuala ya Ukimwi,
Kifua Kikuu, Malaria na Magonjwa yaliyosahaulika.
Uteuzi
huu umetangazwa rasmi na Dk. Chan wakati wa kikao cha 68 cha Baraza Kuu la Shirika
la Afya Duniani kilichoanza tarehe 14 hadi 26 Mei, mwaka huu, Geneva nchini
Uswisi.
Dk.
Mpanju-Shumbusho ni mtaalamu na kiongozi mwenye uzoefu wa miaka zaidi ya 30
katika ngazi za juu za uongozi katika sekta ya Afya na Ushirikiano wa
Kimataifa.
Kabla
ya uteuzi huu, Dk. Mpanju-Shumbusho alikuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu Msaidizi
ndani ya Shirika la Afya Duniani upande wa Ukimwi, Kifua Kikuu, Malaria na Magonjwa
yaliyosahaulika na akiwa na cheo cha Ukurugenzi wa Idara inayoshughulikia
Ushirikiano wa Shirika la Afya Duniani na Mfuko wa Dunia wa kupambana na
Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria (Global Fund to Fight AIDS, Tuberculosis na
Malaria).
Dk.
Mpanju-Shumbusho pia ni mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani kwenye Bodi ya
Mfuko wa Dunia wa kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria na Bodi
mbalimbali za kimataifa.
Hapo
awali, Dk. Winnie Mpanju-Shumbusho alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya kudhibiti Ukimwi
na magonjwa mengine katika WHO, Makao Makuu Geneva, Uswisi.
Kabla
ya kujiunga WHO, aliwahi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa East, Central and Southern
Africa Health Community Secretariat yenye makao makuu yake, Arusha, Tanzania.
Vilevile,
aliwahi kuwa Mkuu wa Idara na Mhadhiri Mwandamizi, Idara ya Afya ya Jamii na
Mgonjwa ya Watoto, Chuo Kikuu cha Dar
es Salaam, (Muhimbili University of Health Science).
Katika
wadhifa huu, Dk. Winnie pia alikuwa mwanzilishi wa mipango mbalimbali ya afya
na taaluma na Mshauri Mkuu wa Wizara ya Afya,
Tanzania upande
wa Afya ya Jamii. Pia amewahi kuwa mjumbe wa Bodi mbalimbali za kimataifa.
Dk.
Mpanju-Shumbusho ana Shahada ya Udaktari kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam; vilevile
ana Shahada ya Uzamili katika Afya ya Jamii kutoka Chuo Kikuu cha Tulane, Marekani
na Shahada ya Uzamili katika Medicine (Paediatric and Child Health) kutoka Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam. Vilevile ana Shahada ya Uzamifu na Shahada nyingine
mbalimbali.
Akiwa
Mkurugenzi na Mtaalamu katika Shirika la Afya Duniani, amekuwa mstari wa mbele
kuandaa, kuongoza na kutekeleza mipango mkakati ya Dunia ya kujenga na
kuimarisha sekta ya afya, hususani katika nchi maskini na zinazoendelea.
Mipango
hii imezaa mafanikio makubwa ikiwamo kujenga uwezo wa nchi maskini kukabiliana
na maradhi na afya za kina mama na watoto.
Sambamba
na hilo, mipango
hiyo pia ilifanikisha upatikanaji wa dawa za gharama nafuu katika nchi maskini
ili kuweza kumudu gharama za matibabu kwa watu maskini.
Nchini
Tanzania,
Dk. Mpanju-Shumbusho ameweza kufanikisha upatikanaji wa matibabu na huduma
nasaha za kusaidia kudhibiti ugonjwa wa Ukimwi, Kifua Kikuu, Malaria na
magonjwa yaliyosahaulika.
Dk.
Shumbusho ameolewa na ana watoto wawili, wa kiume na kike.
No comments:
Post a Comment