DAR ES SALAAM
Chama cha Wamiliki/Waendeshaji wa Mitandao ya Jamii nchini
'Tanzania Bloggers Network' - TBN kilichosajiliwa rasmi na Serikali Aprili 2015
na kupewa namba ya usajili; S. A 20008 kinapenda kuwajulisha wanaotaka kujiunga
na chama hicho kuwa fomu za kujiunga zinatolewa.
Wahusika ni wamiliki na
waendeshaji wote wa mitandao ya kijamii (blogs na forums) Tanzania na
Watanzania wanaofanya kazi kama hiyo nje ya nchi.
Sifa kuu kwa mwanachama ni kuwa na blog ambayo ina umri wa
miezi sita tangu ianze kuendeshwa mfululizo ambayo ipo hai. Kwa wakazi wa Dar
es Salaam wenye sifa na wanataka kujiunga na TBN fomu zinapatikana kwenye Ofisi
za Muda za Tanzania Bloggers Network (TBN) kwenye Jengo la Dar Free Market
lililopo mkabala na Barabara ya Ally Hassan Mwinyi.
Mwanachama muitaji wa kujiunga kabla ya fomu atatakiwa kutoa
shs 25,000/- ikiwa ni Kiingilio cha mwanachama, shs 15,000/- yakiwa ni malipo
ya ada ya miezi mitatu kwa mwanachama na shs 10,000/- ikiwa ni malipo ya kadi
ya TBN kwa mwanachama (utambulisho). Jumla kuu kila mwanachama anatakiwa kulipa
shs 50,000/- na kupewa risiti halali ya malipo ya TBN.
Fomu zitatolewa siku za
kazi kuanzia saa nne asubuhi hadi saa kumi jioni. Zoezi la utoaji fomu
litasimamiwa na Mweka Hazina wa TBN, Shamim Mwasha (0767418941). Fomu pia
zinapatikana Ofisi za Michuzi Media Group, mjini Jengo refu karibu na Hospitali
ya Ocean Road ghorofa ya pili.
Kwa wanachama wa mikoani juu na namna ya kujiunga wasiliana
nasi kwa barua pepe; mushijoa@gmail.com au piga namba;
0756469470.
Kwa wanaoitaji kujiunga mnaombwa kuchukua fomu mapema kabla
ya zoezi la usaji lililoanza 22 Aprili, 2015 halijafungwa.
NB;- Kwa watakaohitaji katiba ya TBN watapewa pia ofisini
coppy, lakini coppy hiyo wataigharamia wenyewe. Hata hivyo utaratibu unafanywa
wa kuichapa kwenye soft coppy katiba hiyo na itatumwa mikoani kwa gharama za
TBN.
Imetolewa na:
Joachim Mushi, 0756469470
Mwenyekiti wa Muda wa Tanzania Bloggers Network (TBN)
No comments:
Post a Comment