Mtendaji Mkuu Bodi ya Ligi, Boniface Wambura akimkabidhi Kombe nahodha
wa timu ya Harmburg Queens Jamila Kassim baada ya kuwa mabingwa katika michuano
ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars mkoa wa
kisoka wa Ilala. Hafla ya kukabidhi kombe ilifanyika jana katika uwanja
wa Kumbukumbu ya Karume Jijini Dar-es-Salaam.
Wachezaji wa timu ya Mchanganyiko FC
wakishangilia baada ya kuwa mabingwa katika michuano ya vijana chini ya
umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars mkoa wa kisoka wa Kinondoni.
Hafla ya kukabidhi kombe ilifanyika jana katika uwanja wa Kumbukumbu ya
Karume Jijini
Dar-es-Salaam.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Michuano
ya soka kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Aitel Rising Stars kwa
mikoa ya kisoka ya Ilala, Kinondoni na Temeke jana ilifungwa
rasmi
katika uwanja wa Karume ambapo mabingwa wa mikoa husika walikabidhiwa
zawadi zao.
Kwa
upande wa wasichana, Hamburg Queens walifanikiwa kutawazwa mabingwa wa
mkoa wa Ilala huku Bombom wakitwaa taji la ubingwa wa mkoa huo kwa
upande wa wavulana.
Katika
mkoa wa Temeke upande wa wasichana, timu ya Evergreen ndio walitangazwa
mabingwa na Wakati Ujao ndio walioibuka wababe kwa upande wa wavulana
katika mkoa huo.
Kwa mkoa
wa Kinondoni, timu ya wasichana ya Mburahati Queens walifanikiwa kuwa
mabingwa wakati Mchanganyiko FC wakitangazwa
mabingwa
kwa upande wa wavulana.
Akizungumza
wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi, Meneja Uhusiano wa
Airtel Tanzania Jackson Mmbando, alitoa shukrani zake za dhati kwa
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) pamoja na vyama vya mikoa kwa
ushirikiano wao ambao unawapa nguvu ya kuendelea kudhamini programu hiyo
ya soka kwa vijana.
“Mwaka
huu tumeshuhudia uboreshaji mkubwa zaidi wa mashindano haya baada ya
ujio wa timu za wasichana ambao wameongeza msisimko wa michuano hii. Pia
naamini tutapata wavijana wenye vipaji ambao watasaidia kutangaza taifa
letu hapo baadaye katika ngazi za
kimataifa”,
alisema Mmbando.
“Shukrani
zangu nazipeleke pia kwa Makatibu wa mikoa shiriki kwa kufanikisha
kupata vijana bora na wenye weledi ambao ni nuru ya taifa
letu kwa
siku za usoni”, aliongeza.
Kwa
upande wake mgeni rasmi, Boniface Wambura ambaye ni Mtendaji Mkuu wa
Bodi ya Ligi, alisema anaipongeza Airtel kwa mchango wao hapa nchini wa
kuvumbua vipaji vya vijana ambao ni manufaa kwa taifa kwa siku za
baadaye.
“Nimefarijika
kuona vijana wakijituma na kucheza kwa ari kubwa licha ya umri wao
mdogo, jambo ambalo litawafikisha mbali katika maisha yao ya soka, kitu
cha msingi ni kuhakikisha hamkati tama ili kuweza kufikia malengo”
alisema Wambura.
“Sisi TFF, tutahakikisha michuamo yote
inayohushisha vijana inaendeshwa kwa weledi wa hali ya juu ili kupata
vijana bora watakaoweza kulisaidia taifa letu kuanzia timu za vijana
mpaka za wakubwa hapo baadaye”, Wambura aliongeza.
Wakati
huo huo mikoa hiyo mitatu ya kisoka jana imeanza kutoana josha katika
mashindano ya Airtel Rising Stars yenye lengo la kupata
mabingwa
wa mkoa wa Dar es Salaam chini ya Chama cha Mpira wa soka mkoani wa Dar
es Salaam (DRFA).
Katika
michezo miwili iliyochezwa jana timu ya Ilala Girls iliibuka na ushindi
mnono wa magoli 4-1 dhidi ya Temeke Girls wakati timu ya
wavulana,
Ilala Boys walipepetana na Temeke Boys ambapo Ilala Boys waliibuka na
ushindi wa mabao 2-0.
Mashindano ya Airtel Rising Stars ambayo mwaka huu yanashirikisha
mikoa ya Ilala, Kinondoni, Temeke, Morogoro, Mbeya, Mwanza na Arusha inatarajiwa
kuingia kwenye hatu nyeti ya fainali za Taifa iliyopangwa kufanyika
kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam, kuanzia Septamba 11 hadi 21.
No comments:
Post a Comment