Meneja
Huduma kwa Jamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi (katikati), akiongea na
wawakilishi wa kikundi cha MIRANACO katika hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa
mbalimbali vitakavyowasaidia katika biashara yao ya ufugaji wa nyuki vikiwemo
mizinga ya nyuki 20, mashine za kukamulia asali 1, vifaa vya kinga ya nyuki 2,
chupa za lita 1 400, chupa za asali za lita 5, 200 na zana zitumikazo kuboresha
biashara ya ufugaji wa nyuki mjini Mbeya . Wakishuhudia kutoka kulia ni
Mtangazaji wa kipindi cha FURSA Irine Paul akifuatiwa na Meneja mauzo wa Airtel
mkoani Mbeya Saidi Zani
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
MBEYA
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel
imewawezesha vijana wajasiriamali wa kikundi cha MINARACO kutoka mkoani Mbeya
wanaojishughulisha na ufugaji wa nyuki. Kikundi hicho kinaundwa na vijana 76
walioamua kuungana na kujihusisha katika ufugaji wa nyuki ili kujikwamua na
changamoto za maisha. Kupitia mradi wa Airtel FURSA kikundi hicho kimewezeshwa
kwa kupatiwa mizinga ya nyuki 20, mashine za kukamulia asali 1, vifaa vya kinga
ya nyuki 2, chupa za lita 1, 400, chupa za asali za lita 5, 200 na zana
zitumikazo kuboresha biashara ya ufugaji wa nyuki
Akikabidhi vifaa hivyo meneja wa huduma
kwa jamii wa Airtel Bi Hawa Bayumi alisema, “vitendea kazi waliopatiwa ni
vyakisasa zaidi na vitasaidia kuboresha ufugaji huo na kuwawezesha vijana hao
kupata mavuno zaidi ya waliokuwa wakipata awali”.
Akiongezea amesema, “mpango huo wa
kuwawezesha wajasiriamali vifaa ni sehemu ya mpango wa kampuni ya Airtel wa
kuwawezesha vijana ili kuboresha maisha yao na ya watu wanaowazunguka”.
“Sisi kama Kampuni ya mawasiliano tumeona
ni vizuri kushirikiana na wajasiriamali na hasa vijana wenye umri kati ya miaka
18-24 ili kuhakikisha tunawawezesha na kukuza mitaji yao ya biashara kwa
mafunzo na vifaa” alisema meneja huyo”.
Wakipokea msaada huo wameishukuru, Airtel
kwa kujitoa kwa kuwasaidia vijana katika kutatua changamoto zinazowakabili na
kuahidi kutumia vifaa hivyo kwaajili ya kuongeza uzalishaji ili kufikia malengo
waliojiwekea katika kikundi hicho.
“Hatukuamini kuwa Airtel itakuja
kututembelea, kuangalia mahitaji yetu na hasa kwa kutupatia msaada wa vifaa vya
kisasa walivyo tupatia leo, tunawashukuru sana na tunaahidi kutumia vyema
msaada huu ili kuhakikisha tunakuza na kuendeleza ufugaji bora wa nyuki”
alisema mwakilishi wa kikundi hicho John Maige.
Akiongezea Maige alisema, “Awali
tulikuwa na changamoto ya uchache wa mizinga, vifungashio vya asali na soko la
uhakika, lakini Airtel imetusaidia kwa kutupa mafunzo na vifaa vya kutosha
vitakavyo tusaidia kupata Asali ya kutosha na yenye ubora mzuri “.
Kampuni ya simu ya Airtel inazunguka nchi
nzima kukutana na vijana kwa lengo la kuwapa elimu ya ujasiriamali na kisha kutoa
uwezeshaji kwa vijana.
No comments:
Post a Comment