Tangazo

September 21, 2015

Selcom yaleta mfumo mpya na wa kisasa wa malipo ya tiketi za tamasha la “KILIFEST"







Kwa mara ya kwanza nchini Tanzania wahudhuriaji wa tamasha la ‘KiliFest’ wataweza kutumia Selcom Card kupata tiketi za tamasha hilo lililoandaliwa na kampuni ya Bia ya Kilimanjaro Premium Lager ambalo litafanyika siku ya Jumamosi September  26, 2015 katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es salaam.

Kati ya mawakala wa Selcom zaidi ya 15,000 wanaopatikana nchi nzima ni mawakala 40 tu wameochaguliwa kuuza tiketi za KiliFest kwenye vituo vyao na wote hao wanapatikana Dar es salaam.

 Baada ya kulipia Tsh 10,000/- tiketi itawekwa moja kwa moja kwenye Selcom Card kwa njia ya kielektroniki ambapo mteja atakuwa amepata Selcom Card bure na atatakiwa kufika na kadi h

Selcom Card itamuwezesha mteja kupata tiketi za tamasha la KiliFest kwa sasa na kuitumia kadi hiyo hapo baadae kufanya malipo na manunuzi mbalimbali baada ya tamasha hilo.

Malipo na manunuzi yatakayoweza kufanyika kwa kutumia Selcom Card ni pamoja na malipo ya manunuzi ya bidhaa kwenye supermarkets, kulipia mafuta ya gari kwenye vituo vya mafuta, kulipia tiketi za matamsha yajayo, kulipia bili za chakula kwenye migahawa/bar, kupokea na kutuma pesa kwenda mitandao yote na kwenye akaunti za benki, kutoa pesa kwa wakala wa Selcom, kulipia tiketi za usafiri, bili za LUKU, DAWASCO, NHC, AzamTV, ZUKU, Startimes, DSTV,  nk, kununua vifurushi vya internet pamoja na muda wa maongezi wa mitandao yote.

Hapo awali kumekuwa na changamoto kubwa wakati wa uuzaji wa tiketi za matamasha mbalimbali ambapo imekuwa ni vigumu kudhibiti wizi na tiketi feki, kwa kupitia mfumo huu mpya wa Selcom Card sasa waandaji wa matamasha wataweza kuzuia wizi wa tiketi na kuwa na uwezo wa kuuza tiketi mapema kabla ya tamasha na pia kuweza kujua nani ameingia kwenye tamasha hilo.

Lengo kuu la Selcom Card ni kuwarahisishia wananchi na kuwajengea utamaduni wa kufanya malipo mbalimbali kwa kutumia mfumo wa kadi ambao ni wa haraka, salama na uhakika bila kubeba fedha mkononi kila wanapohitaji kufanya malipo au mununuzi.  Watumiaji wataweza kuongeza fedha kwenye kadi zao za Selcom (Salio) kwa mawakala wote wa Selcom nchini au kwa njia ya simu banking.

Selcom ni kampuni inayoongoza katika utoaji wa huduma mbalimbali za kifedha kwa njia ya simu za mkononi na yenye uzoefu mkubwa kwenye nyanja ya Teknolojia nchini Tanzania na ndio msingi wa uendeshaji wa huduma ya kifedha kwa njia ya simu ikishirikiana na mitandao yote minne ya simu hapa nchini, benki zaidi ya 30 na vituo vya mauzo vya Selcom vinavyotumia mashine za POS vilivyopo zaidi ya 15,000 nchi nzima. Pia Selcom ni wawezeshaji wa malipo na manunuzi ya huduma mbalimbali kwa washirika zaidi ya 50 kupitia simu za mkononi, simu banking na mawakala wake.  

Selcom ni kampuni inayoongoza Tanzania kwa kuanzisha huduma za malipo ya kielektroniki katika miji mbalimbali ya Afrika Mashariki na ni kampuni ya kwanza kuzindua malipo na manunuzi kwa njia ya kadi nchini Tanzania.

Selcom, Tunakuwezesha Kwa Njia Ya Teknolojia


SEHEMU ZINAPOPATIKANA TIKETI ZA KILIFEST

NO.
SHOP NAME
LOCATION
DECRIPTION
1
Village Super Market
Masaki
Sea Cliff House Branch
2
Village Super Market
Masaki
Chole Road Branch
3
Village Super Market
Mbezi Beach
Tank Bovu Branch
4
Shrijee Supermarket
Osterbay - Morogoro Store near Mohans
Osterbay Branch
5
Shrijee Supermarket
Masaki
Masaki Branch
6
Shrijee Supermarket
Kisutu - Mtendeni Street
Kisutu Branch
8
Shoppers Supermarket
Mikocheni - Shoppers Plaza
Mikocheni Branch
9
Shoppers Supermarket
Mbezi Beach - Kwa Street
Mbezi Beach Branch
10
A to Z Supermarket
Upanga - Ocean Road - Near Ocean Road Hospital
Ocean Road Branch
11
Imalaseko Supermarket
Posta - Pamba Street
Posta Branch
12
Koli Finance
Posta - J Mall/Habour View Tower/Samora Street
J Mall Branch
13
Puma Petrol Station
Kisutu - Jamuhuri Street
Kitumbini Branch
14
Bahamadi Shop
K/koo - Living stone/Agrey Street
Opposite Bakhressa Depot
15
Bahamadi Shop
K/koo - Mahiwa/Living Stone Street
Nearby Kariakoo Bazar Bulding
16
Habibu Shop
K/koo - Living stone/Pemba Street
Opposite Green Bureau Change
17
Crown and Beauty  Shop
Mlimani City
In Mlimani City Mall
18
Big Bon
Sinza Mori
At the Big Bon Petrol Station
19
C - Park Cub
Kinindoni B
Kinondoni B nearby Bus Stop
20
Baby Face Internet Café
Mwananyamala (A)
Near bus stop of Mwannyamala A
21
Treenaz G.Supplies
Kawe - Mlalakuwa Street
Opposite EFM Radio
22
Jukas Shop
Africa Sana
Opposite Africana Shop near the Africana Market
23
Puma Petrol Station
Mbezi Bech Branch
Between Interchick and Tank Bovu Bus Stops
24
Petro Fuel Station
Tegeta Branch
Near Azania Bus Stop
25
Swai Shop
Ubungo Riverside
At kibangu Bus stop
28
Virus Internet Café
Magomeni - Magomeni Mapipa
Nearby Mapipa Bus Stop
29
Bakari Shop
Magomeni -Mwembe Chai
Neaby Bus Stop Opposite Mosque
30
Twaha Shop
Magomei – Kagera
Nearby Old Kagera Bus Stop
31
Eshanaa Classic Ware
Magomeni - Kagera
Opposite Oil Com Petrol Station
32
Elvis Digital & Network
Mbezi Louis
Dealer of DSTV opposite Old Bus Stop
33
Mohamed Shop
Mbagala Kongowe
Nearest to the Bus Stop of Tua Ngoma
34
Merseytel Shop
Mbagala Rangi Zakiem
Opposite Darlive Pub
35
Kipanga Stationery
Mtoni kwa Aziz Ally
Nearby Aljazira Supermarket
36

No comments: