Wafanyakazi wa Airtel wakiwa katika picha ya pamoja na makombe yao mara
baada ya kukabithiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya viwanda na Biashara
Uledi Abbas Musa mara baada ya kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel kuibuka
washindi katika vipengele mbalimbali katika maonyesho Biashara ya Afrika
Mashariki ya mwaka huu.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
· Yazawadia vikombe vinne vya ubora wa huduma na bidhaa
Mwanza
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imepokea vikombe vinne
katika maonyesho ya Biashara ya Afrika Mashariki kufatia ubora
wake katika kutoa huduma na bidhaa za kibunifu kwa wateja wake.
Maonyesho haya ya Biashara ya Afrika Mashariki ni maarufu kwa kuonyesha
aina mbalimbali za bidhaa ikiwemo bidhaa za matumizi ya kawaida
na ya viwanda, huduma, mashine na teknologia. Na maonyesho haya
yametoa fulsa ya kukutanisha wadau pamoja na kubadilishana uzoefu wa
kibiashara na kuwawezesha ushirikiano wa biashara katika nchini za
ukanda wa mashariki.
Akiongea wakati wa halfa hiyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na
Biashara, Uledi Abbas Musa alisema” Maonyesho haya yana lengo la kuwapatia
makampuni yaliyoko katika ukanda wa Afrika ya Mashariki fulsa ya
kujitangaza na kukuza biashara zao lakini pia kuwapatia nafasi ya
kuboresha mahusiano ya kudumu na wateja wao. Leo najisikia furaha
kuwazawadia kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kuonyesha ubora
wake katika huduma, bidhaa, tecknologia za kibunifu na kwa kuwa washindi
wapili katika maonyesho ya mwaka huu”
Aliongeza kwa kusema” Airtel imedhihirisha dhamira yake ya kutoa huduma
za kibunifu na za uhakika za mawasiliano ya simu za mkononi na kutokana
na hilo tumeona ni muhimu kuwapongeza na kuwazawadia kwa jitihada zao”
Kwa upande wake Afisa Masoko na bidhaa wa Airtel , Bwana Emmanuel
Raphael alisema” huu ni mwaka watano mfululizo sasa kwa Airtel kushiriki
katika maonyesho haya tukuwa na lengo la kufikia wateja wetu, kutoa
elimu ya huduma na bidhaa tunazotoa pamoja na kuboresha
mahusiano
nao. Maonyesho haya pia yamekuwa ni fulsa muhimu kwetu kuonyesha bidhaa
na huduma zetu za kibunifu na za kisasa na pia ni nafasi
pekee ya kushikiana na makampuni mengine yanayoshiriki kila mwaka”
“Napenda kuwashukuru waandaaji wa maonyesho haya
kwa kutambua na kuona mchango wetu na tunahaidi kuendelea na dhamira
yetu ya kutoa huduma bora na za kibunifu zinazokidhi mahitaji ya wateja
wetu.” Aliongeza Raphael
Katika halfa hiyo, Airtel ilipokea makombe manne ya ubora katika vipengele
vya namba moja kwenye kutoa huduma, namba moja katika sekta ya
mawasiliano, namba moja katika teknologia ya mawasiliano ya habari na
namba mbili katika maonyesho ya mwaka huu. Nchi zilizo shiriki katika
maonyesho ya mwaka huu ni pamoja na Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda and
Burundi.
No comments:
Post a Comment