Mratibu wa Veta kanda ya Dar es Salaam Bi. Frorence Kapinga akiwakaribisha wakuu wa vyuo vya ufundi vyenye usajili wa awali wa VETA kanda ya Dar es Salaam kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Msimbazi jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Dar es Salaam. Bw.Habibu Bukko akizungumza jambo wakati wa mkutano la wakuu wa vyuo vya ufundi pamoja na kumkaribisha mgeni rasmi kwa ajili ya ufunguzi wa kutano huo.
Mgeni rasmi Mwalimu Charles Philemon akizungumza na wakuu wa vyuo na wawakirishi wao(hawapo pichani) wakati alipokuwa anafungua mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Msimbazi jijini Dar
Bw. Asanterabi Kanza ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa VETA kanda ya Mashariki akiwasilisha mada kwa wakuu wa vyuo pamoja na wawakilishi wao(hawapo pichani) waliofika kwenye mkutano huo ili kukumbushana mmbo ya msingi kwenye uendeshaji wa vyuo hivyo vya ufundi.
Mkutano ukiendelea
Wakuu wa vyuo wakifuatilia kwa umakini kinachoendelea kwenye mkutano huo
Picha ya Pamoja
Na Mwandishi wetu
Kongamano la wakuu wa vyuo pamoja na wamiliki wa vyuo vya
ufundi stadi kanda ya Dar es Salaam lafanyika jijini Dar es Salaam kwa ajiri
ya kupeana maelekezo kwa vyuo vilivyo
pata usajiri wa awali ili waweze kupata
usajiri wa kudumu vilevile kupewa hisibati na namna gani waweze kufuata taratibu
ili kupata usajiri huo wa kudumu.
Mwenyekiti wa bodi ya VETA kanda ya Dar es Salaam
Mwalimu Charles Philemon akiongea na
wamiliki na wakuu wa vyuo vya ufundistadi kuhusiana na wamiliki hao kupata
usajili wa kudumu kwani wao kama VETA familia wanauhitaji wa kutambua na haki
ya kupata hisibati inayoonyesha aina ya
kozi zinazotolewa na chuo husika kilichopo katika mfumo wa VETA, pia alisema wana mambo muhimu ambayo yanayopaswa kukumbushana ni pamoja na wanayotekeleza, kwani wao nia yao ni kutoa mafunzo kwa wanafunzi kwa uhakika ili wao waweze kuwa mabalozi wazuri katika kazi zao wawapo nje , tuendelee kujenga mambo ya stadi za kazi katika vyuo vyetu ili kuwahakikishia wananchi kuwa tunaendelea kutoa wakufunzi wenye sifa zinazostahili lakini yote haya yanatokana na kuwa na chuo chenye usajili wa uhakika na wakufuata taratibu za mamlaka ya VETA.
Kwani watu mbalimbali hupimwa kutokana na stadi zao
mbalimbali wanazozipata katika vyuo
vyetu na kwenda nazo katika kuzitekeleza
maeneo tofauti , watu hao ambao wamepita kupitia katika mafunzo ya ufundi stadi VETA ndio watu wenye stadi za kazi kwani
hutenda kazi kutokana na elimu na utashi mkubwa wanaoupata katika mafunzo yao kupitia
vyuo mbalimbali vyenye usajili wa VETA. anasema “kutokana
na semina zinazoendelea najua sisi ni familia moja hata kama katika familia
kuna watoto warefu na wengine wafupi lakini wote ni watoto wa VETA tufanye kazi
kwa umoja ili kutoa vitu vilivyobora zaidi kutofautisha na aina nyingize za
utoaji mafunzo, kwani ninaamini walimu wenye ubora ndio wanaopatikana katika
mamlaka ya VETA”
Pia aliweza kusisitiza fursa ya kujengana kwa kutembeleana
baina ya chuo kimoja na chuo kingine kwa ajiri ya kupata ufanisi zaidi katika mafunzo mbalimbali pamoja na fani kwani familia
inajengwa kwa kuwa na uhusiano mzuri na uzuri wa familia huonekana ndani ya
VETA ni pale watu mnavyofaidika katika mambo mbalimbali iwe kwa
kujengana na kusaidiana kwa kuinua kile kinacho patikana kwani muda mwingi huwa tunakutana mara moja katika maonesho
mbalimbali lakini familia hii ya VETA ni mamlaka inayo unganisha vyuo
mbalimbali.
Naye mkurugenzi wa VETA
kanda ya Dar es Salaam Bwana Habibu Bukko alisisitiza kuhusiana na kusajiliwa pamoja na
kupata Hisibati itakayo saidia katika vyuo vyetu, hivyo aliweza kusema baada ya
kupata usajili ndani ya miezi kumi na mbili (12) ni lazima kila chuo kiwe
kimepata hisibati kwa wale wote waliokamilisha usajili huo wa mafunzo ya
ufundi stadi, pia aliweza kuzungumzia nini maana ya ambapo alisema HISIBATI ni kutambua zile
fani ambazo zinatolewa na chuo au umahili wachuo chako upo kwenye fani zipi.
No comments:
Post a Comment