Kikosi cha brasband cha Magereza kikiongoza Maandamao kuelekea uwanjani kwenye mahafali hayo ya Kumi na Tatu ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) na ya Tatu kwa kampasi ya Mbeya . |
Baadhi ya wahadhiri wa Taasisi hiyo ya Uhasibu (TIA) Kampasi ya Mbeya wakiandamana kuelekea uwanjani tayari kwa mahafali hayo . |
Wahitimu wakiwa katika maandamano hayo ya Mahafali ya kumi na Tatu ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) na ya Tatu kwa Kampasi ya Mbeya. |
Baadhi ya wahitimu wa Uhasibu (TIA) kampasi ya Mbeya |
Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania Dkt .Joseph Kihanda akizungumza kwenye mahafali ya Kumi na tatu ya Taasisi na ya Tatu kufanyika katika Kampasi ya Mbeya . |
Mgeni rasmi Ndugu Nyirembe Munasa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Mbeya ambaye pia alimwakilisha Waziri wa Fedha katika mahafali hayo ya Taasisi ya Uhasibu (TIA) Kampasi ya Mbeya. |
Wahitimu wa Masomo ya Uhasibu Katika Taasisi hiyo wakisikiliza kwa umakini nasaha kutoka kwa mgeni rasmi . |
Kikundi cha ngoma za asili kutoka Ilemi jijini Mbeya kikitoa burudani katika mahafali hayo . |
Mgeni rasmi Nyirembe Munasa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Mbeya akitoa zawadi kwa washindi walio fanya vyema katika masomo yao. |
Baraza la Taifa la
Elimu ya
ufundi (NACTE)limetoa kibali kwa taasisi ya Uhasibu Tanzania
(TIA)
kampasi ya
Mbeya ili kuongeza kozi nyingine za shahada ya Masoko na
uhusiano
kwa umma
(Bachelor Degree in Marketing and public Relation kwa mwaka
wa masomo
wa
2015-16.
Aidha
baraza
hilo pia limetoa kibali kwa kuanzishwa kwa kozi nyingine ya
shahada ya
uhasibu wa
fedha za umma (Bachelor Degree in Public Sector Accounting
and
Finance)
kwa mwaka huu wa masomo.Kauli hiyo imetolewa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania Dkt.Joseph Kihanda kwenye mahafali ya kumi na Tatu ya Taasisi na y a tatu kufanyika katika kampasi ya Mbeya.
Amesema katika mwaka wa masomo wa
2014-2015
kufuatia maombi ya muda mrefu ya wadau wake kampasi ya mbeya
ilianza
kutoa kozi
za shahada ya uhasibu na shahada ya Ununuzi na Ugavi ambazo
mwitikio
wake
umekuwa mkubwa hivyo kulazimika kuomba kibali cha kuanzisha
kozi nyingine
ambazo
tayari baraza hilo limekwisha toa kibali.
Amesema kuanzishwa kwa kozi hizo
kumeiwezesha
kampasi ya Mbeya kuwabakiza wanafunzi wanaohitimu kozi za
Stashahada
katika fani husika ambao hapo awali walilazimika kuhamia
vyuo vingine
vinavyotoa
kozi hizo kwenye ngazi ya shahada na hivyo kuikosesha
Taasisi
mapato.
Aidha Dkt Kihanda amesema kuwa kuanza kwa
kozi hizo
pia kutawawezesha wakazi wa mbeya na mikoa mingine
ya jirani
kupata
fursa ya kujiendeleza kitaaluma Katika ngazi ya
shahada kwani
masomo
yanatolewa katika mfumo wa kutwa na jioni hivyo kukidhi kiu
ya wengi.
Hata hivyo amesema kampasi ya mbeya
imejiimarisha
sana katika utoaji wa elimu yenye ubora ili kuwawezesha
wahitimu
kufanya
vizuri katika masomo yao ya baadae na katika sehemu zao za
kazi.
Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi ya ushauri ya wizara ya fedha Profesa Isaya Jairo amesema bodi hiyo itashirikiana na uongozi wa TAASISI kuishauri wizara ya fedha kuitngea fedha za kutosha kwa ajili ya kuboresha miundo mbinu mbalimbali pamoja na vitendea kazi.
Katika mahafali hayo, jumla ya wanafunzi 1689 wa stashahada na stashahada za udhamili katika fani mbalimbali wanahitimu masomo yao ambapo kati yao wasichana 851 na wanaume 838.
(Imeandaliwa na Emanuel Madafa Jamiimojablogu Mbeya)
Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi ya ushauri ya wizara ya fedha Profesa Isaya Jairo amesema bodi hiyo itashirikiana na uongozi wa TAASISI kuishauri wizara ya fedha kuitngea fedha za kutosha kwa ajili ya kuboresha miundo mbinu mbalimbali pamoja na vitendea kazi.
Katika mahafali hayo, jumla ya wanafunzi 1689 wa stashahada na stashahada za udhamili katika fani mbalimbali wanahitimu masomo yao ambapo kati yao wasichana 851 na wanaume 838.
(Imeandaliwa na Emanuel Madafa Jamiimojablogu Mbeya)
No comments:
Post a Comment