Afisa uhusiano na mwandamizi wa Baraza la
Sanaa la Taifa (BASATA), Aristed Kwizera (kushoto) akimuaga mshindi wa
Airtel Trace Music Stars,
Mayunga Nalimi kwa ajili ya kwenda kurekodi mziki na kupata mafunzo
toka kwa mwanamuziki wa kimataifa Akon nchini Marekani ,katika
hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika katika makao makuu ya ofisi ya Airtel
Morocco jijini Dar Es Salaam. Anayeshuhudia (katikati) ni Afisa
uhusiano wa Airtel Tanzania jane matinde .
XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX
Nalimi Mayunga ,
mshindi wa shindano la Airtel Trace Music Stars Afrika, ameondoka nchini
Jana kuelekea nchini Marekani kwa lengo la
kupata
mafunzo na kurekodi nyimbo yake Nalimi mayunga ameondoka jana Jumatatu
usiku na kwenda kufanya kazi na nguli wa mzuki wa R&B nchini
Marekani Bwana Akon ambapo anatarajiwa kukaa muda wa wiki moja kisha
kurejea nyumbani tarehe 24 Novemba.
Akiongea
wakati halfa ya kumuaga, Afisa habari mwandamizi wa Baraza la Sanaa la
Taifa (BASATA), Aristide Kwizera alisema” Tunajisikia furaha kuona
vijana wa kitanzania wakitangaza sanaa na nchi yetu duaniani kupitia
muziki. Napenda kumpongeza sana mayunga kwa kupata ushindi ambao
umempatia nafasi hii nono na kumwomba atumie vyema fursa hii.
Sisi kama
wadau wakuu wa sanaa nchini tunawapongeza sana Airtel kwa kuanzisha
program zenye lengo la kukuza sanaa na muziki wa nchini kama hii ya
Airtel Trace Music Stars na nyingine nyingi.
Naye
mshindi wa shindano la Airtel Trace Music Stars Afrika, Nalimi Mayunga
alisema” ile siku niliyokuwa naisibiria kwa hama leo imefika
na
nimejipanga kuondoka kwenda kujifunza mengi na ya msingi katika maisha
yangu ya muziki . Naamii safari hii itakuwa ni ya mafanikio makubwa
na mwanzo wa hatua yangu ya mafanikia katika tasinia ya muziki Napenda
kuwaambia watanzania wajiandae kusikia kibao na video kali ntakayoifanya
na Akon kwani nimejiandaa vya kutosha kuhakikisha nashirikiana nae
vyema ili tunatoa nyimbo kali itakayowapa burudani wapenzi wa muziki
pande zote duniani.
Aliongeza Mayunga Kwa upande wake
Aliyekuwa jaji katika shindano la Airtel Trace Music Stars
Tanzania na Mwalimu wa Muziki Tony Joet alisema” Mayunga
amekuwa akifanya mazoezi kujiandaa kwa deli hii toka alipotangazwa
mshindi wa Airtel Trace Afrika. Ninaimani naye kwani ameonyesha uwezo mkubwa
na nidhamu ya hali ya juu na naamini atafika mbali na namtakia kila
laheri katika safari yake”.
Akiongea kwa niaba ya Airtel Afisa
Uhusiano wa Airtel, Bi Jane Matinde alisema” mipango yote ya
safari imekamilika na mayunga atakuwa marekani
kwa muda wa wiki moja, tunaamini mayunga atakaporejea atakuwa tofauti
kabisa na alivyokwenda na ndio hasa lengo letu sisi Airtel, kuwawezesha
na kuwainua vijana kubadilisha maisha na kufikia malengo yao.
Shindano
la muzuki la Airtel Trace Music stars lilizinduliwa Oktoba 2014 na huu
ndio msimu wa kwanza wa shindano hili ambalo limewapatia
vijana
watanzania na waafrika nafasi ya kuonyesha vipaji vyao na kupata fulsa
mbalimbali za muziki.
No comments:
Post a Comment