Wanakijiji wa Mtaa wa Ng’ong’ona manispaa Dodoma wakiangalia banda
alilokabidhiwa Kijana Fikiri Chinji (hayupo pichani) anayejishughulisha
na ufundi seremala, pamoja na msaada wa vifaa mbali mbali vya ufundi kupitia
mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, mwishoni mwa wiki hii.
XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX
· Airtel FURSA
kusaidia kikundi cha wajasiliamali 30 Dodoma
Airtel kupitia mpango wake
wa Airtel FURSA umeendelea na utekelezaji wa ahadi yake ya kuwawezesha
wajasiliamali wawili kila wiki nchini kwa kutoa misaada yenye thamani ya hadi
shilingi milioni 10 kwa kikundi au kijana atakaeotoa mchanganuo na kusimamia biashara
itakayoweza kusaidia kuongezea kipato na kupunguza umasikini katika jamii .
Wiki hii Airtel FURSA
imeingia mkoani Dodoma na kukabidhi vitendea kazi vyenye dhamani ya
shilingi milioni 9 kwa kijana mjasiliamali Fikiri Chinji anaeishi katika
kijiji cha Ng”ong”ona ili aweze kuendeleza shughuli zake za useremala na kuweza
kuajiri vijana wengine wanaomzunguka.
Akizungumza wakati wa
hafla fupi ya makabidhiano katika kijiji cha Ng”ong”ona Dodoma Afisa
Uhusiano wa Airtel Bi Dangio Kaniki alisema “vifaa alivyoomba ndio
tunavyomkabidhi ni pamoja na mashine yakupiga msasa, mashine kwaajili ya
kutobolea na kutengeneza urembo pamoja na nyingine yakuranda mbao. Pia
tumejenga kalakana yake hapa kijijini ili apate mazingira mazuri ya kufanyia
kazi zake kwa ustadi na kufundisha vijana wengine kujiajiri kupitia mradi
huu”
“Airtel Fursa tumeona ni
muhimu kumuwezesha kijana huyu aweze pia kuongeza thamani ya vitu
anavyotengeneza na kuviuza kwa bei nzuri, vile vile tumejipanga kuja tena
Dodoma hivi karibuni na tutasaidia kikundi cha ujasiliamali kiitwacho PAMBANA
cha Dodoma Mjini chenye jumla ya vijana 30 ambapo wasichana ni 20 na wavulana
10 na kinajishughulisha na usafi wa mazingira na kutengeneza sabuni” alieleza
Dangio
Akipokea Vifaa hivyo huku
akishangiliwa na wanakijiji wenzake, kijana Fikiri ameishukuru Airtel
fursa kwa kuona umuhimu wa kumpiga jeki kwa kumwezesha vifaa na sehemu ya
kufanyia shughuli zake,
“Sasa nitafanya kazi zangu
kwa ufanisi mkubwa ikiwa ni pamoja na kutengeneza bidhaa zitakazokubalika
sokoni, naishukuru sana Airtel Fursa kwa kunishika mkono” Alisema Fikiri
Mradi wa Airtel FURSA uko
katika msimu wa pili ambapo tokea kuanzishwa kwake umefanikiwa kuandaa na
kufanya semina za ujasiliamali 17 na kukutana na vijana wenye umri kati ya
miaka 18 hadi 24 zaidi ya 3000, pia hadi sasa imeweza kutoa misaada kwa vijana
na makundi ya vijana hao wajasiliamali zaidi ya 108 kwa lengo
kuwaongezea uzalishaji na kipato.
No comments:
Post a Comment