Tangazo

March 16, 2016

Fastjet yaongeza safari Dar es Salaam – Nairobi


                

Dar es Salaam

 Shirika la ndege la gharama nafuu Afrika, Fastjet Tanzania limeongeza idadi ya safari zake  kwenye njia yake ya Dar es Salaam  na Nairobi ikiwa ni mwitikIo  mkubwa kwa mahitaji ya abiria.

Kuanzia Machi 21 fastjet itakuwa inafanya safari zake mara mbili kwa siku kwenda na kurudi  kati ya miji hiyo miwili  kila siku  ndani ya wiki na hivyo kufanya safari zake  kuwa ni 28 kwa wiki kati ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam na Uwanja wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta  jijini Nairobi.

Shirika hilo ambalo hadi sasa  linafanya safari moja kila siku  kati ya miji hiyo miwili, limeongeza masafa yake ya kuruka  ili kuwapatia abiria huduma nzuri nyakati za asubuhi na jioni.

Kwenye safari ya asubuhi, ndege itakuwa inaondoka Dar es Salaam saa 12.00 na kutua Nairobi saa 1.20. Aidha, safari ya kurudi itaanza saa 1.50 na itatua Dar es Salaam saa 3.15.

Aidha, safari mpya za jioni ndege itakuwa inaondoka  Dar es Salaam saa 2.15 na kutua Nairobi saa 3.35. Safari ya kuridi ndege itaondoka Nairobi saa 4.05 na itatua Dar es Salaam saa 5.30.

Kupanuka kwa  ratiba hiyo kutawezesha kusafirisha takribani  abiria 19,000 kila mwezi  kupitia safari za fastjet  kati ya hiyo miji miwili, na hivyo kuwapa wasafiri njia nzuri zaidi  na mbadala wa safari kwa nauli wanayoimudu.

 “Kila mara tumekuwa tunaahidi  kuongeza masafa yetu ya  njia yetu kati ya Dar es salaam na Nairobi kutokana na mahitaji ya wateja kuongezeka kunakosababisha na nauli wanayoimudu, usalama, kasi na huduma kwa wakati,” alisema Meneja Mkuu wa Fastjet Tanzania, John Corse.

Aliongeza: “Idadi ya watu jijini Dar es Salaam na Nairobi kwa pamoja ni zaidi ya milioni themanini  ambao wengi wao walishindwa kusafiri kwa ndege kutokana na ukubwa wa nauli  na hivyo tunaamini iliwatenga sehemu kubwa ywa watu dhidi ya usafiri wa anga lakini hivi sasa wana chaguo la ndege la uhakika na wanalolimudu.”

Corse anabainisha kuwa tangu fastjet ianze  kufanya safari zake  kati ya Dar es Salaam na Nairobi inakadiriwa kuwa theluthi moja ya abiria wake  ni mara yao ya kwanza  kutumia usafiri huo  ambao vinginevyo walikuwa wanashindwa kumudu nauli ya kusafiri kwa njia ya anga kati ya miji hiyo miwili.

 “Kutangazwa kwa safari 14 za ziada kwa wiki ikiwa ni miezi miwili tu baada ya fastjet kutangaza kuanza kwa safari za anga kati ya nchi  hizi mbili Januari 11, 2016 kunaonesha msisitizo wa kuongezeka kwa idadi ya wateja ambao wanaweza kuifikia usafiri wa anga wanaoumudu. Kwa hakikika hili linaonesha matokeo chanya kwenye maisha ya wananchi na hali kadhalika kwenye kukua kwa uchumi baina ya nchi hizi mbili,” alisema Corse.

Tiketi kwa ajili ya safari hizo za ziada  kutoka Dar es Salaam tayari ziko kwenye mauzo ambapo  nauli inaanzia  shilingi 168,000 za Tanzania kwa safari moja (bila kodi ya shilingi 102,900) kwa kuondokea Tanzania, ambapo fastjet inashauri abiria wake  kukata tiketi zao mapema kwa ajili ya siku wanayotaka kusafiri ili kunufaika na nauli zake za chini na nafuu.

Aidha, tiketi kwa ajili ya safari hizo za ziada kutoka Nairobi nazo tayari ziko kwenye mauzo, nauli zinaanzia  kwenye dola za Marekani  120 kwa njia moja (bila kodi ya dola za Marekani 40) kwa kuondokea Kenya, na vile vile fastjet inawashauri  abiria kukata tiketi mapema  kabla ya siku ya kusafiri ili kunufaika na tozo hiyo ya nauli ya chini.

 “Safari za ziada za kurudi jioni inamaanisha kwamba abiria wanaweza kupanga ama wakutane Dar es Salaam au Nairobi, na kusafiri hadi kwenye maeneo yao jijini na kurudi nyumbani siku hiyo hiyo,” anasema Corse na kuongeza, “njia hii na chaguo hili sahihi ni muhimu kwa abiria ambao ni wafanyabiashara ambao wanakuwa kwenye shinikizo la kubana muda na kuokoa gharama, na ambao  hawataki kulala nje ya maskani yao kwa siku moja au mbili.”

Matokeo ya safari za fastjet  kwenda na kurudi nchini Kenya  tayari ni makubwa ; ambapo Corse anadokeza kuwa  siku ambayo fastjet ilitangaza kuwa itaanzisha safari za anga kati ya Tanzania na Kenya kwa bei nafuu ilisababisha mashirika pinzani ya ndege kushusha nauli zao kwa asimilia 40.

 “Kimsingi ukweli unabakia kwamba ushindani ni mzuri kwa wateja. Huwapa chaguo  na husababisha nauli kushuka. Nauli wanayoimudu kunafanya iwe rahisi kwa wajasiriamali wengi, watalii na wageni wengine  kusafiri kati ya Tanzania na Kenya,” alisema Corse.

Hali kadhalika kitu kingine kilichopo kwenye njia hizi mbadala ni kuboresha mizigo inayobebwa na abiria wa fastjet, ikijulikana kama ‘Freighty’ ambayo inamruhusu abiria  kusafirisha  hadi kilo 80 kwenye mabegi yaliyokaguliwa kwa  shilingi za Tanzania 84,000. Njia hii mbadala kimsingi imekuwa maarufu  miongoni mwa wafanya biashara wanaosafiri na fastjet kwenye kununua  bidhaa za jumla za kimataifa  kwa ajili ya kwenda kuuza kwenye masoko yao ya nyumbani.

Ukataji wa tiketi unaweza kufanyika kwa njia ya mtandao www.fastjet.com, kupitia wakala wa usafiri  aliyethibitishwa na  fastjet au kwa kuwasiliana na fastjet  kwa njia ya simu +255 784 108 900.  Malipo kwa ajili ya tiketi yanaweza kufanyika kwa fedha taslim, kwa njia ya mtandao au malipo kwa njia ya simu za mkononi.

No comments: